Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chino 'wana man' afunguka kolabo yake na Fid Q

Leo msanii nguli wa hip hop 'Fid Q' Farid Kubanda ameposti kwenye kupitia akaunti yake ya Instagramposti mbili zilizoleta maswali mengi ya kwanza ni tweet ya Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA na posti ya pili ni mazungumzo yake na mwanamuziki Issaya Mtambo 'Chino Kidd'

Tweet ya MwanaFA inasema "Siku nikisikia FidQ kwenye beat ya amapiano ndio ntakubali imetushinda moja kwa moja" FidQ akasema "Tuombe tusifike huku"

Posti ya pili imeonyesha mazungumzo ya Whatsap yanasema "My brother Fid Q mambo vipi kakangu mdogo wako hapa Chino wanaman nina chuma changu kipya hapa nikisikiliza naona kabisa hii amapiano unahitajika wewe humu yani naomba nibariki Sauti yako tuu humu Kakaangu"

Mwanaspoti imemtafuta mwanamuziki Chino nakumuuliza kuhusiana na yeye kutaka kutoa wimbo na FidQ pia ameona tweet ya MwanaFA

"Niwe mkweli sijaiona tweet ya MwanaFA na nimepata taarifa baada ya kuapata wazo la kufanya wimbo na FidQ lakini sijajua anamaana gani"