Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bonny Mwaitege asikitishwa kuzushiwa kifo

Muktasari:

  • Mwaitege amezungumza na Mwanaspoti akisema yeye ni mzima wa afya na amesikitishwa na kushangazwa na uzushi huo wa kifo akibainisha anapigiwa simu nyingi na watu wake wa karibu akiulizwa kuhusu suala hilo.

MSANII wa nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii.

Mwaitege amezungumza na Mwanaspoti akisema yeye ni mzima wa afya na amesikitishwa na kushangazwa na uzushi huo wa kifo akibainisha anapigiwa simu nyingi na watu wake wa karibu akiulizwa kuhusu suala hilo.

"Aisee pole sana dada yangu, mimi ni mzima wa afya njema, sijafa. Huu ni uzushi tu wa watu. Kwa kweli nimesikitika sana. Nimeanza kupigiwa simu na watu kutokea Nairobi na Dar na mikoa mingine, hii ni mbaya sana, hapa sasa hivi nipo njiani naelekea Nairobi kwenye kazi za Injili Mungu ni mwema," amesema Mwaitege.

Mwanaspoti lilimuuliza pia kuhusu madai kwamba ametengeneza kiki akidaiwa ana kanisa lake, akasema sio kiki kwani kwa hatua aliyopo yeye si mtu wa kuhitaji kufanya kiki anapofanya jambo lake.

"Kwanini nifanye kiki? Yaani kiki ndio nijiue mwenyewe? Kwa hatua niliyofikia ya kazi ya sanaa yangu sio ya kufanya kiki ndio nifanye kitu," amesema Bonny.

Kwa upande wa mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha, amezungumza na Mwanaspoti kuhusu uzushi huo wa kifo cha Bonny Mwaitege akisema alizisikia taarifa hizo na kwamba ziliwaathiri watu wengi.

"Hizi habari mimi niliziona tu kwenye mitandao, ni habari ambazo sio nzuri kabisa, kuna baadhi ya watu wanamzushia kifo mtu kwa maslahi yao tu. Hii habari ya Bonny Mwaitege imewaathiri watu wengi sana kitu ambacho sio kizuri," amesema Flora.

Bonny Mwaitege ametamba na nyimbo nyingi zikiwemo kama 'Safari Bado', 'Dunia Dunia', 'Acha Nizaliwe', 'Bado Nampenda' na 'Mke Mwema' ambao zimempatia umaarufu mkubwa.