Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi lebo... Kutoka wasanii kibao hadi ziro

LEBO Pict

Muktasari:

  • Ila sasa wasanii maarufu Bongo ndio wanashikilia biashara hiyo lakini changamoto kubwa imekuwa ni namna wasanii wanaowasaini wanavyojitoa katika lebo au lebo hizo kushindwa kuwasimamia vizuri.

KATIKA miaka ya hivi karibuni mastaa ndio hasa wamekuwa wakianzisha rekodi lebo ikiwa ni tofauti na hapo awali ambapo biashara hiyo ilitawaliwa sana na watayarishaji muziki kupitia studio zao wakitegemea faida kupitia mauzo ya kanda.

Ila sasa wasanii maarufu Bongo ndio wanashikilia biashara hiyo lakini changamoto kubwa imekuwa ni namna wasanii wanaowasaini wanavyojitoa katika lebo au lebo hizo kushindwa kuwasimamia vizuri.

Hapa tunakuletea orodha ya lebo chache za mastaa Bongo ambazo zilisaini wasanii zaidi ya wawili ila kwa sasa wote wameondoka kwa sababu mbalimbali na kuwaacha wamiliki peke yao, yaani wakitoka hatua ya kuwasimamia wasanii kadhaa hadi sifuri.

LB 01

The Industry (Navy Kenzo)

Kundi la Navy Kenzo liloanzishwa mwaka 2013 baada ya kuvunjika kwa Pah One, ndio wamiliki wa The Industry ambayo mnamo 2016 ndipo ilianza rasmi kuwatambulisha wasanii wake ambapo iliwatoa watatu kwa mpigo, Seline, Wildad na Rosa Ree.

Ila Oktoba 2017, Rose Ree akatangaza kuachana na The Industry na pia hao wengine nao waliondoka kipindi hicho ikiwa ni takribani mwaka mmoja wa kufanya kazi pamoja, na lebo hiyo ilionyesha kuwekeza sana maana video za wasanii wote zilifanyika nje ya nchi.

Baada ya miaka mitatu, The Industry walimsaini msanii mwingine, The Great Eddy aliyetoka na EP yake, Small Bad Wolf (2021) ila naye tangu wakati huo hajasikika popote na hata  lebo hiyo haipo katika uwanja wa kusimamia wasanii. 

Kati ya wasanii wote waliosainiwa The Industry, Rosa Ree ndiye amefanya vizuri zaidi akitoa albamu moja, Goddess (2022) na kushinda tuzo tatu tofauti zinazomtaja kama Msanii Bora wa Hip Hop, ameshinda EAEA 2022, The Orange Awards 2022 na TMA 2022.

LB 02

Unity Entertainment (AY)

AY aliyetoka na ngoma yake, Ni Raha Tu (2001), mwaka 2012 aliwasainii wasanii watatu, Ommy Dimpoz, Stereo na Feza Kessy chini ya kampuni yake, Unity Entertainment ambayo ilijikita katika kusimamia na kufanya promosheni ya kazi za wasanii.

Hata hivyo, Feza Kessy, mshiriki wa Big Brother Africa Tha Chase 2013 na mtangazaji wa zamani wa Choice FM, ndiye alikuwa msanii wa kwanza kujitoa katika menejimenti hiyo, kisha wakafuata Ommy Dimpoz na Stereo.

Utakumbuka kabla ya Stereo kujiunga na Unity Entertainment, alifanya kazi na M Lab (Music Laboratory) ambayo ndio ilimtoa kimuziki akitamba na albamu yake, African Son (2011).

Na chini ya Unity Entertainment, Ommy Dimpoz alitoa wimbo, Tupogo (2014) akimshirikisha J Martins kutokea Nigeria, huku Stereo akitoa Wako (Never Let You Down) (2014) akiwa na Victoria Kimani wa Kenya, msanii wa kwanza wa kike kusainiwa Chocolate City.

LB 03

SMG (QuIck Rocka)

Rapa Quick Rocka aliyetoka na ngoma yake, Bullet (2010) baada ya kusainiwa MJ Records, naye baadaye alifungua studio yake na kuazisha lebo, Switch Music Group (SMG) ambayo ililisaini kundi la OMG lenye wasanii watatu.

Kundi la OMG lililoundwa na Young Lunya, Conboi na Salmin Swaggz huku Quick Rocka akiwapa OMG (Ooh My God) jina hilo baada ya kuona uwezo wao ni mkubwa upande wa kuchana.

Marapa hao watatu walifanya vizuri wakati huo wakitoka na ngoma yao, Uongo na Umbea (2017) wakimshirikisha Barakah The Prince lakini baadaye lebo iliamua kusitisha mkataba nao kwa madai ya kushindwa kurejesha uwekezaji uliofanyika.

Ikumbukwe naye Quick Rocka alikuwa ndani ya kundi la Rockaz akiwa na wenzake watatu, Chief  Rocka, Dau Rocka na Mo Rocka lakini ni yeye pekee aliyepata nafasi ya kusainiwa MJ Records baada ya Master J kuvutiwa na uwezo wake kufuatia kumsikia redioni.

LB 04

Mdee Music (Vanessa Mdee)

Lebo hii ilianza kusaini wasanii Februari 2017 wakianza na Mimi Mars aliyetoka na wimbo wake, Sugar (2017), alipokewa vizuri hadi kupewa nafasi katika jukwaa la Coke Studio Africa kama Msanii Bora Chipukizi 2018.

Baada ya Mimi Mars, Mdee Music walimsaini Briana Simba ambaye alimshirikisha Vanessa katika wimbo wake, Silence (2018), ila haikuchukua muda mrefu Briana Simba akaondoka katika lebo hiyo kwa madai ya kumaliza mkataba wake.

Na pindi Vanessa ambaye ndiye mwanzilishi wa lebo hiyo alipotangaza kuachana na muziki hapo Juni 2020 ndio ukawa mwisho wa Mdee Music kwani Mimi Mars kwa sasa anafanya muziki wake kivyake na sio chini ya lebo kama hapo awali.

Kwa mujibu wa Mimi Mars akiongea na podcast ya Swahili Radio by Audiomack, lebo hiyo pia ilishindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa mtaji wa kutosha baada ya Vanessa kujiweka kando.

LB 05

Konde Music Worldwide (Harmonize)

Baada ya kuachana na WCB Wasafi, Harmonize alitangaza kuanzishwa kwa Konde Music Worldwide hapo Oktoba 2019, na kufikia Aprili 11, 2020 wakamsaini msanii wa kwanza ambaye ni Ibraah, na ndani ya muda mfupi wakawa na jumla ya wasanii sita.

Hata hivyo, kuanzia Januari 2022 wasanii walianza kuondoka hadi Mei 2025 wakawa wameondoka wote ambao ni Country Wizzy, Cheed, Killy, Anjella, Young Skales na Ibraah, mwanamuziki aliyetamba na kibao chake, Nitachelewa (2020).

Utakumbuka Ibraah ndiye alikuwa wa kwanza kusainiwa na akawa mwisho kuondoka akiwa ametoa EP mbili, Steps (2020), Karata 3 (2021) pamoja na albamu moja, The King of New School (2022).

Na sasa Konde Music imebaki na Harmonize peke yake kama mwanzilishi na mmiliki kama ilivyo kwa wasanii wengine hapo juu, Navy Kenzo, AY, Qui  ck Rocka, Vanessa Mdee ambao nao waliingia katika biashara ya lebo ila sasa wameipa kisogo.