Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Emmanuel Mbasha avunja ukimya, amtaja Flora

MBASHA Pict

Muktasari:

  • Flora Mayala alipotafutwa juu ya tetesi hizo alisema ndoa yake ni imara na kuomba atafutwe kufafanua zaidi, japo hakupatikana tena, ila moja wa rafiki zake alisema taarifa hizo zilimshtua hata yeye, ila wawili hao wapo ndio maana walikuwa wakitalii mbugani.

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amevunja ukimya na kuanika sababu zilizomfanya asimame kuhusiana na masuala ya muziki huo, huku akimtaja aliyekuwa mkewe Flora inayoelezwa ndoa aliyokuwa nayo imepatwa misukosuko.

Akizungumza na Mwanaspoti hivi karibuni akiwa mkoani Kigoma, Mbasha alisema kwa sasa yuko bize na kufanya biashara ya madini ambayo ilikuwa ndoto yake siku nyingi.

“Sijaacha kufanya muziki, ila kwasasa nimesimama kwa muda sitaki kufanya chochote kinachohusiana na muziki badala yake nafanya biashara ya madini ambayo ilikuwa ni ndoto yangu tangu muda mrefu,” alisema Mbasha.

Mwanaspoti lilimbana na kumuuliza juu ya taarifa zilizoibuka mtandaoni hivi karibuni kuhusu ndoa ya zilipendwa wake alisema:

“Mimi na Flora hatuzungumzi na wala sina mawasiliano naye hata kwa salamu, yaani kwa sasa kila mmoja ana maisha yake, kwa ishu ya kuandika ameachika mimi nimeandika tu (kicheko),” alisema Mbasha kila kutoa ufafanuzi.

Flora Mayala alipotafutwa juu ya tetesi hizo alisema ndoa yake ni imara na kuomba atafutwe kufafanua zaidi, japo hakupatikana tena, ila moja wa rafiki zake alisema taarifa hizo zilimshtua hata yeye, ila wawili hao wapo ndio maana walikuwa wakitalii mbugani.