Basata yamuita mezani Ney wa Mitego

Friday May 07 2021
ney pic
By Nasra Abdallah

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemuita mezani msanii Ney wa Mitego, ili kusikiliza hoja zake wapi hajaridhika.

Wito huo umetolewa leo Ijumaa Mei 7, 2021 na Ofisa Sanaa wa baraza hilo, Bona Masenge, hilo katika kipindi cha XXL cha Clouds ambapo walikuwa wakieleza masuala mbalimbali ya Sanaa ikiwemo kujibu maswali ya  sakata linaloendelea la kukagua nyimbo za wasanii.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita siku moja tangu msanii huyo kueleza kutaka kujitoa Basata na kuanza kusambaza kazi zake mtaani bila kupitia Basata.

Akizungumzia hilo, Bona amesema kama Basta wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Ney kwani alienda kwenye jamii kulalamika wakati shughuli hiyo ya ukaguzi ilikuwa bado haijakamilika na ndio mana alipewa maelekezo ya kwenda kuirekebisha.

Pia amesema kamati ya maudhui inayopitia nyimbo sio kwamba ndio chombo cha mwisho kwani kuna nafasi ya kumtaka msanii kwenda mbele kama hajaridhika, lakini Ney hakupitia hatua hiyo.

Hata hivyo ofisa huyo amesema kwa Ney   amesema lengo lilikuwa kuupangia wimbo wake daraja, lakini alionekana kutokubali hili.

Advertisement

Bila kutaja ni maneo gani haswa yalikuwa na ukakasi katika wimbo huo, ofisa huyo alisema ni wimbo ambao unapaswa kuwa na muda wa kusikilizwa.

Aidha Bona amesema katika ukaguzi huo , Ney alituma mwakilishi na hawajui alienda kumpa ujumbe gani mpaka kupata hasira kwenda kulalamika kwa umma bila kuwasiliana nao kwa kuwa kama ni barua ya nini alitakiwa afanye walimpa na alichopaswa kufanya ni kwenda kuonana nao kama hakuridhika.

Wakati kuhusu kukuta watu wachache wanaofanya kazi hiyo ya ukaguzi na kuchukua hadi saa tisa kumaliza shughuli hiyo, walisema halina ukweli wowote na kueleza licha ya uchache hakuna msanii ambaye alishawahi kushindwa kukaguliwa kazi yao na kueleza kama yupo ajitokeze.

“Licha ya uchache wetu, kwa wimbo mmoja huwa inawachukua dakika tano kukaguaa na kueleza kwa siku wanaweza kukagua hata nyimbo 12 na kama ikatokea zikafika nyingi kwa ajili ya ukaguzi huongeza watu,”amesema

Aidha ili kuepuka gharama, Ofisa Sanaa huyo aliwashauri wasanii kupeleka wimbo kabla hawajaumalizia kwa ajili ya kutoka  ili kuepuka gharama  kwani wanachofanya ni kulinda maadili.

Advertisement