Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Babu Seya aukataa uhuni dansini

BABU Pict

Muktasari:

  • Akipiga stori na Mwanaspoti, mkongwe huyo aliyewahi kuwika na bendi mbalimbali ikiwamo Marquis Original, Sambulumaa na Achigo Band, aliasema, jamii inaamini idadi kubwa ya wanamuziki wanajihusisha na vitendo vya kihuni kutokana na umaarufu na kupata fursa ya kukutana na watu wengi.

NGULI wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ amepinga madai kwamba wanamuziki wa miondoko ya dansi kuwa ni wahuni.

Akipiga stori na Mwanaspoti, mkongwe huyo aliyewahi kuwika na bendi mbalimbali ikiwamo Marquis Original, Sambulumaa na Achigo Band, aliasema, jamii inaamini idadi kubwa ya wanamuziki wanajihusisha na vitendo vya kihuni kutokana na umaarufu na kupata fursa ya kukutana na watu wengi.

“Si kweli kwamba wanamuziki wa dansi ni wahuni, uhuni ni tabia ya mtu tangu awali isipokuwa anakuwa hajapata mahali pa kuonyesha tabia hiyo sasa anapokuja katika muziki anafungua makucha,” alisema Nguza na kuongeza;

“Wapo wanamuziki wengi si wahuni na hadi leo wana heshima zao, hii ni kazi kama zilivyo kazi nyingine tatizo tunafuatiliwa sana na vyombo vya habari kutokana na aina ya kazi yetu.”

Mkongwe huyo aliyewahi kukabiliwa na kesi ya ubakaji na kuhukumiwa kifungo kabla ya kutolewa kwa msamaha wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, alisema hata katika kazi nyingine uhuni unafanyika kwa nafasi kubwa lakini wanamuziki wanafuatiliwa kwa kuwa ndilo kundi linalowakusanya watu wengi katika jamii.

Babu Seya bado analia na masilahi ya wanamuziki na anaweka wazi kuwa akipata bahati ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Sukuhu Hassan atamsisitizia kuweka mkazo katika kuhakikisha haki za wasanii haziibiwi.

“Nikipata bahati ya kukutana na Rais, neno langu litakuwa moja tu, asimamie haki zetu, watu wanatuibia kupita kiasi na matokeo yake wengi tunakufa masikini, tunabaki na umaarufu.”