Baba Diamond atoa majibu kuhusu Diamond kutokuwa mtoto wake

Friday January 15 2021
New Content Item (1)
By Nasra Abdallah

Abdul Juma Issack, ambaye inafahamika kuwa ndiye baba mzazi wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuhusu kauli ya mama wa msanii huyo kuwa si mtoto wake.

diamondi pic 2

Akihojiwa kwa njia ya simu katika kipindi cha Mashamsham, leo Januari 15, 2021 mama wa Diamond anayejulikana kwa jina la Sandra, aliweka wazi kwamba baba mzazi wa msanii huyo ni mzee anayefahamika kwa jina la Salum Iddi Nyange na mzee Abdul anabaki kuwa baba mlezi tu.

diamond pic1

Kutokana na kauli hiyo, Mwanaspoti ilimtafuta mzee Abdul kujua namna alivyoipokea kauli hiyo.

Katika maelezo yake, amesema hata yeye amefurahi kusikia hilo kwa muhusika kuliongea kwa kuwa hata yeye mwenyewe alikuwa hajielewi wala hajitambui.

Advertisement

“Madhari muhusika kashaongea hivyo sawasawa kabisa,”amesema.

Alipoulizwa kwanini zamani aliwahi kuulizwa suala hilo lakini akakataa amesema “Si mmeshapata jibu kwa mwenyewe mnataka mimi niseme nini tena wakati yeye ndio aliyebeba mimba.”

“Tunajua wanawake wengi kwa sasa wana makadi ya kliniki hadi matatu manne kila moja na baba yake huku wakiangalia mwanaume mwenye maslahi,” alisema.

Pia amesema hata yeye anakubali kwamba Diamond sio mtoto wake japokuwa amelijua leo baada ya mama yake kuliongelea na kuongeza kuwa sasa ndio anapata majibu kwa nini mtoto huyo alikuwa hamuhudumii na amekubali matokeo.

“Yule mtoto sio riziki yangu, kwani nimembeba tangu anatoka hospitali, tukamlea na tukagombana alipokuwa kidato cha kwanza sijawahi kusikia hayo.”

DIAMOND MUMY PIC

Hata hivyo Mwanaspoti ilitaka kujua labda mama huyo kaamua kutoa kauli hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo vya kumlalamikia kila uchwao kuwa hamuhudumii, baba Diamond amesema kwake sio lazima kuhudumiwa wala msanii huyo kuwa mtoto wake.

Advertisement