Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ATM YA WIKI: P.Diddy Utajiri wake balaa

Muktasari:

  • Sasa imeibuka kwa mkali wa Hip Hop na mmiliki wa lebo ya muziki ya Bad Boy Entertainment, Mmarekani mwingine mweusi, Sean Love Combs ‘P Diddy’ ambaye kwa sasa yupo mahabusu akisubiria kuanza kusikilizwa kwa kesi zake kadhaa zinazomkabili.

LOS ANGELES, MAREKANI: NDIYO hivyo, hata mbuyu hufika wakati ukaanguka. Ndivyo inavyotokea kwa watu wengi. Ilianza kwa O. J. Simpson, Bill Cosby, R Kelly na wengine wengi na hasa wakihusishwa na kesi za unyanyasaji wa kingonohao wote ni Wamarekani weusi.

Sasa imeibuka kwa mkali wa Hip Hop na mmiliki wa lebo ya muziki ya Bad Boy Entertainment, Mmarekani mwingine mweusi, Sean Love Combs ‘P Diddy’ ambaye kwa sasa yupo mahabusu akisubiria kuanza kusikilizwa kwa kesi zake kadhaa zinazomkabili.

Kama ilivyo kwa mastaa waliotajwa hapo juu waliotumikia na wanaotumikia kifungo pamoja na wengine, wamefanya kazi kubwa kwenye muziki na kutengeneza pesa nyingi za kuwawezesha kutamba kokote, kuwekeza kwenye biashara na mambo mengine.

Diddi ni mmoja wa mastaa waliofanya makubwa kwenye muziki na kutengeneza pesa ndefu na mara kadhaa amekuwa akitajwa na Jarida la Forbes kama msanii wa Hip Hop tajiri zaidi duniani, akichuana na mastaa wengine kama Jay Z, Dr Dre, Kanye West na wengine.

Je unajua Diddy alipataje utajiri wake?


ANAPIGAJE PESA

Asilimia kubwa ya pesa zake anapata  kupitia muziki na kwa mwaka 2022 pekee aliingiza Dola 50 milion zaidi ya Sh100 bilioni, pia kwa wastani tangu alipoanza muziki hadi sasa kila mwaka alikuwa akikunja zaidi ya Dola 60 milioni kutokana na uuzaji wa albamu zake na malipo ya shoo.

Pia ana kampuni yake ya kudizaini na kutengeneza nguo iitwayo “Sean John,” aliyoianzisha mwaka 1998. Diddy pia ndiye bosi wa kampuni ya Combs Enterprises, inayojihusisha na uwekezaji kwenye biashara mbalimbali.

Ukiondoa hiyo pia alikuwa ana hisa kwenye kampuni ya viwanywaji ya Ciroc vodka na televisheni ya Revolt TV.

Akishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali aliwahi kuinunua kampuni ya Aquahydrate, mwaka 2019 na kuwa mwekezaji mkuu wa kampuni ya PlayVS.

Amewahi kuigiza katika  muvi mbalimbal kama Made (2001), A Raisin in the Sun (2008), Get Him to the Greek (2010), Draft Day (2014) na The Defiant Ones (2017), huko anakadiriwa kupata zaidi ya Dola 20 milioni katika muvi zote.

Hadi mwaka 2023, alikuwa na utajiri unaofikia Dola 1 bilioni ambao unamfanya kuwa msanii tajiri zaidi wa kiume kwenye Hip Hop  baada ya Jay Z.

MSAADA KWA JAMII

Mwaka 2003 alianzisha mbio zilizochangia zaidi ya Dola 2 milioni ambazo zilienda kutumika kusaidia shule na watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Amekuwa akifanya kazi na taasisi mbalimbali zinazosaidia jamii kwenye matatizpo mbalimbali, kama vile watu wanaoishi na kansa, Ukimwi na walemavu.

Katika taasisi hizo, Diddy anakadiriwa kutoa misaada ya zaidi ya Dola 5 milioni kila mwaka.


MJENGO

Septemba 2014, Diddy alilipa Dola 39 milioni kwa ajili ya kununua nyumba iliyokuwa kwenye eneo la ukubwa kilomita za mraba 17,000, Holmby Hills, huko Los Angeles.

Jumba hilo la kifahari lina bwawa la kuogelea, sehemu ya kutazamia  sinema yenye viti 35, chumba cha mvuke, chumba cha masaji, saluni na chumba cha kunywea viwanyaji mbalimbali.

Pia mwaka 2009 Diddy alilipa Dola 5.25 milioni kwa ajili ya kununua  nyumba ya aliyekuwa mzazi mwenzake, marehemu Kim Porter, aliyefariki mwaka 2018.

Aliiuza nyumba hiyo mwaka 2022 kwa Dola 6.5 milioni.

Vilevile mwaka  2021, msanii huyu alitoa Dola 35 milioni kwa ajili ya kununua nyumba kwenye kisiwa cha Miami inayopatikana kwenye eneo la ukubwa wa hekari 1.3.

BATA NA MAISHA

Hadi sasa ana watoto saba  na mtoto wake wa kwanza alimpata mwaka 1993 na mwanamama Misa Hylton-Brim, akapata watoto wengine wawili wakike na mmoja wakiume aliozaa na Kimberly Porter aliyekuwa naye kwenye mahusiano kuanzia mwaka 1994 na 2007. Pia alipata mtoto mmoja na Sarah Chapman, ,mwaka 2007 aliingia kwenye mahusiano na Cassie Ventura walioachana mwaka 2018.

Mtoto wake wa sana alimpata Oktoba 2022, ambapo alizaa na Dana Tran.

Jamaa ni mtu wa bata na hivi kariuni amekuwa akitafutwa na mamlaka Marekani juu ya kesi ya unyanyasaji wa kijinsia inayomkabili.