20 kuchuana Mr na Miss PSJ Dar

Dar es Salaam. Washiriki 20 kutoka chuo cha Uandishi wa Habari cha Practical School of Journalism, wanatarajia kushiriki mashindano ya Mr and Miss PSJ 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari, leo Novemba 23, 2023, Mratibu wa mashindano hayo, Rahma Mkande alisema lengo la onyesho hilo ni sehemu ya jitihada za chuo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo na kuibua vipaji vipya katika tasnia ya urembo na mavazi.
Alisema mashindano hayo yatafanyika Novemba 24, 2023 katika fukwe ya Ununio Denisty iliyopo Wilaya ya Kinondoni.
Alisema mgeni rasmi katika shindano hilo, anatarajia kuwa mkuu wa wilaya ya kinondoni Saad Mtambule, huku mkuu wa wilaya ubungo Hashimu Komba, akiwa ni mgeni mualikwa.
Alifafanua zawadi watakazo pewa washibdi hao, Mkande alisema mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapewa zawadi, fedha taslimu pamoja na vyeti, huku washiriki wote wa mashindano hayo nao watapewa vyeti vyenye hadhi ya Ubalozi wa chuo.
Mkande amewahimiza vijana kushiriki mashindano hayo kwa kuwa yatawatambulisha na kupata fursa mbalimbali ikiwemo ya kuwa balozi masuala ya Mazingira na Utalii.