Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni kubadilishana kijiti kama mbio fupi za mapenzi

Muktasari:

  • Wasanii kama wanavyotajwa ni kioo cha jamii, watu wengi hupenda kufuatilia maisha na mambo yao, yakiwamo ya mahusiano.

Wasanii kama wanavyotajwa ni kioo cha jamii, watu wengi hupenda kufuatilia maisha na mambo yao, yakiwamo ya mahusiano.

Inawezekana wapo wengi wanaopitia njia kama zao katika mahusiano, lakini wao kwa kuwa ni kioo cha jamii wanaonekana sana.

Kinachoendelea kwao ni kama mbio fupi za mapenzi, kwani wamekuwa wakibadilishana wapenzi na kuona ni ufahari kufanya hivyo.


Wema, Tunda Vs Whozu

Habari iliyoteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni ni mahusiano kati ya mrembo Wema Sepetu na msanii wa muziki wa Bongofleva, Whozu.

Wawili hawa wanateka vichwa vya habari kwa watu wanaofuatilia maisha ya wasanii kutokana na historia zao.

Tukianza na Whozu, yeye anakuwa mdomoni mwa watu kutokana na kutoka katika mahusiano na video queen maarufu, Tunda na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike kabla ya kuachana na Tunda kuanika hadharani kuwa kwa sasa anatoka na msanii wa muziki wa singeli, Meja Kunta.

Hata hivyo, wawili hao kila mmoja kwa wakati wake wamekubaliana kutozungumzia sababu za kuacha kwao kwa madai ya kumheshimu mtoto wao.

Tetesi za mahusiano yao zilianza kuhisiwa baada ya Tunda kuachia moja ya video akiwa na Meja, ambapo msanii huyu wa singeli naye Julai 14 alibadili jina la profile yake na picha kwa kuiweka akiwa na Tunda na kuandika Tunda zuri.

Sasa ikiwa imepita takribani miezi miwili tangu Tunda kufanya maamuzi hayo, Whozu naye kaamua kumwaga ugali kwa kuweka wazi mahusiano yake na mrembo Wema.

Hawa nao walianza kama utani kwa kuweka challenge za kuimba nyimbo za Whozu wakiwa wawili. Whozu alipoulizwa kuhusu hili alisema ni dada yake.


Wema, Hamisa Vs Diamond

Kama kuna msanii amepiga pasi nyingi katika mahusiano ni Wema, kwani baada ya kuachana na msanii anayefanya vizuri kwa kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi, Diamond Platnumz, pasi aliiachia kwa mwanamama mjasiriamli, Zarina Hassan ‘Zari’.

Couple hiyo ilikuwa ikifuatiliwa sio tu Tanzania, bali na chi za Afrika Mashariki kutokana na Zari kuwa raia wa Uganda.

Hata hivyo, Diamond akiwa katika mahusiano hayo, alichepuka na kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, kesi ambayo ilikuwa kubwa lakini waliyamaliza kifamilia.

Hilo likiwa halijapoa vizuri, Diamond alilitibua tena kwa kuonekana wakiwa wanashikana kimahaba na Wema katika siku ya kumtambulisha Mbosso ambaye alikuwa msanii mpya kusajiliwa WCB, hiyo ilikuwa Januari mwaka 2018.

Jambo hili lilimuudhi Zari na kuamua kumwaga manyanga na sasa wamebaki na mahusiano ya mtu na mzazi mwenzie.


Ruby, Aunt Ezekiel Vs Mose Iyobo

Ni mwishoni mwa mwaka 2019, Ruby alipoweka wazi malalamiko kuwa aliyekuwa mpenzi wake na baba wa mtoto wake, Kusah anamnyanyasa kijinsia kwa kumpiga na imefika mahali amechoshwa na vitendo hivyo, huku akiomba msaada kwa vyombo vya sheria kumsaidia.

Hata hivyo ilipofika Januari mwaka jana, Kusah na Aunt waliweka wazi mahusiano yao na hii ilikuwa kwenye arobaini ya mtoto wao wa kiume, huu ukawa mwisho wa uhusiano wa Ruby na Kusah.

Katika kipindi chote ambacho Aunt alikuwa mjamzito, wawili hao walikanusha kuwa na uhusiano.

Ruby naye baada ya kuona hayo, aliamua kumuweka wazi dansa wa Diamond anayeitwa Moze Iyobo kuwa ndiye mpenzi wake.

Ikumbukwe Moze Iyobo ndiye aliyezaa mtoto wa kwanza na Aunt Ezikiel. Hata hivyo mahusiano hayo hayakujulikana yaliishia wapi mpaka leo kwani kila mmoja anaonekana ana hamsini zake.

Hapa ni kama walibadilishana, Aunty akawa na mzazi mwenzake Ruby, ambaye ni Kusah, Ruby akawa na mzazi mwenzake Aunty, Iyobo.


Wolper, Kajala Vs Harmonize

Baada ya mahusiano ya Diamond na wanawake kadhaa kuteka vichwa vya habari, mahusiano mengine yaliyokuwa yanabamba ni ya msanii wa filamu, Jacqueline Wolper na Harmonize ambaye wakati huo alikuwa hajawa mkubwa kisanii kama ilivyo sasa.

Baada ya kuachana, Harmonize alidondokea katika penzi la Sarah, walivyoshindwana akatua mikononi mwa msanii wa filamu Kajala Masanja, ambaye wameshavalishana pete ya uchumba.


Uwoya, Flora Mvungi Vs H Baba

Japo ilikuwa zamani kidogo, lakini ndio hivyo nao walishakuwa katika mahusiano na kuachiana kijiti kama kawaida yao.

Irene Uwoya alikuwa na mahusiano na H Baba akiwa ndiyo katoka kuwa Miss Mwanza na baadaye akaingia katika uigizaji akitingisha na filamu ya ‘Oprah’ ambayo ilimtambulisha kwa mara ya kwanza kwenye ulimwengu wa Bongo movie akiwa na kina marehemu Steven Kanumba na Vicent Kigosi ‘Ray’.

Kama kawaida ya binadamu waliachana kwa sababu wanazozijua wao na H Baba kuzama katika penzi la mwigizaji Florah Mvungi na kufunga ndoa na kujaaliwa kupata watoto wawili na kuachana.


Wanasaikolojia wafunguka

Mwanasaikolojia Charles Nduku anasema haya mahusiano yanayofanywa na wasanii ya kubadilishana ni katika kuwafanya waendelea kuzungumziwa na watu. Wakijua wakiwa na mtu ambaye hayupo kwenye tasnia ya sanaa au asiye maarufu ni rahisi kusahaulika.

Hata hivyo alisema kingine ni kwamba wengi wanaishi maisha ya kuigiza ya kutaka kuonekana wao ni watu fulani, lakini ukweli ni kwamba hawapo hivyo.

“Umaarufu ndiyo unaosababisha haya, wanashindwa kukubaliana na nafsi zao kutoka nje ya boksi,”alisema Nduku.

Kwa upande wa Mshauri Nasihi wa Saikolojia kutoka taasisi ya Health Tanzania, Bosco Bosco alisema ukiangalia kihisia unaweza kuona wasanii hao wamechanganyikiwa, lakini kinadharia wako sahihi na kuongeza kuwa suala la mahusiano lina sababu nyingi.

Aliitaja mojawapo ni mtu huangalia mtu anayemjali, hivyo kama aliyekuwa naye alikuwa hamjali na pia hakukuwa ulinzi wa penzi lake ni wazi atakwenda kwingine. “Lakini atakwenda kwa mtu aliye karibu naye, kwa kuwa wao wasanii lazima watakuwa karibu na wasanii wenzao.

“Mapenzi mazuri ni kuwa na mtu ambaye unamfahamu, hivyo kwa kutoka na wanaofahamiana nao hudumu na yakivunjika huendelea na maisha yao waliyoyazoea, tofauti wangekuwa wakitoka na mtu mwingine asingewaelewa hata kidogo,” alisema Bosco.

Pia alisema mazingira wakati mwingine huwasukuma watu kuwa katika mahusiano, hasa yanayowakutanisha mara kwa mara, kwani inakuwa rahisi kusomana tabia na kutamaniana tofauti na wale wanaoishi mbalimbali.