Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma ya Nani Kama Mama yamtesa Chiristian Bella

Muktasari:

Mwimbaji huyo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amedai kama angekuwa ni Mtanzania kwa kazi za muziki alizofanya ikiwemo Wimbo wa ‘ Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz tayari angekuwa ameshapewa tuzo za muziki.

Tuzo ya Wimbo wa ‘Nani kama Mama’ inaendelea kumtesa Mwanamuziki Christian Bella na kudai kuna mazingira huwa yanajitokeza ya kunyimwa nafasi kwa kuwa yeye sio Mtanzania.

Mwimbaji huyo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amedai kama angekuwa ni Mtanzania kwa kazi za muziki alizofanya ikiwemo Wimbo wa ‘ Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz tayari angekuwa ameshapewa tuzo za muziki.

Bella, alisema hayo baada ya kuulizwa na Mwanaspoti kuwa wimbo wake wa ‘Nani kama Mama’unaendelea kufanya vizuri kwanini hadi leo hajapata tuzo hata moja.

Aidha Bella aliendelea kuweka wazi kuwa, japokuwa wimbo huo hajaupatia tuzo, hata moja kwake umempa nguvu ya kuandaa kazi nzuri zaidi ya alizozitoa na anajiamini muziki anaoufanya unapendwa na wengi, kukosa tuzo hakutamrudisha nyuma, bali kunamfanya aongeze nguvu zaidi ya kufanya muziki mzuri.

“Unajua siku zote najijua kama nafanya kazi nzuri na mashabiki wananikubali kwa kazi zangu. Ila kukosa tuzo hakunivunji moyo, yaani ni sawa na kunizidishia akili ya kufanya vitu vizuri na pia nakubaliana na matokeo, hakuna tatizo lolote la kusema nilalamike, ila nawasihii mashabiki wangu wasivunjike moyo.

“Nina akili ya ziada ambayo Mungu amenipa na heshima ya jinsi ya kuishi, unajua kazi yetu ina mambo mengi, ina fitna, hakuna mtu anayeweza kupenda wewe uwe mbele ukizingatia mimi sio Mtanzania, kuna vikwazo vingi najua, ukiweka hivi wanakubana hapa,” alisema Bella.

Aliongeza, “Yaani namaanisha kama ningekuwa Mtanzania ningekuwa mbali zaidi, kwa sababu sio kwamba sipendwi napendwa sana na mashabiki mpaka na viongozi wa serikali, lakini nadhani kama ningekuwa Mtanzania ningepata fursa nyingi na kuna vitu vingi zaidi ningefanya au ningekuwa mbali zaidi ya hapa nilipo sasa,”alisema.

Wimbo wa‘Nani Kama Mama’ uliingia katika kinyang’anyiro cha Wimbo Bora wa Mwaka 2015 katika Tuzo za Kilimanjaro Music Awards lakini haukuweza kuchukua tuzo na kusababisha mlipuko wa fujo ukumbini Mwanaspoti lilikuwepo ukumbini humo.