Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanaheri anajiamini huyo nyie

MWANADADA anayekimbiza kwenye filamu za Bongo, Mwanaheri Ahmed, ametamba kuwa hakuna mwigizaji wa kike hapa Bongo ambaye anaweza kumwibia mumewe, kwani anamjulia na wanapendana sana na kuaminiana hadi kufikia kufunga pingu za maisha.

“Ninajiamini na ninaimudu ndoa yangu, hivyo huyo mwizi wa kuniibia, ataanzia wapi?” Anasema kwa kujiamini.

“Hakuna mwanamke ambaye anaweza kuniibia mwanaume wangu kipenzi, nasema hakuna.”

Msanii huyo alisema hayo baada ya kuwepo kwa maneno kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzake kudai kuwa huenda wenzie wakamzunguka na kumwibia mumewe, lakini mwenyewe anasema kuwa alishajipanga kabla ya tukio la kuolewa na mumewe aliyemtaja kwa jina moja tu la Hamis.