Mke wa Vardy ,Rooney ni vichambo tu

Thursday October 31 2019

Wayne Rooney ,Jamie Vardy, Rebeccah,Coleen Rooney,burudani,udaku,Michezo blog,Mwanasport,MwanaspotiGazeti,MwanaspotiSoka,

 

By Thomas Matiko

YALE madrama ya mke wa Wayne Rooney na mke wake Jamie Vardy, Rebeccah ni bora sasa yageuzwe Series. Sasa Vardy kampa kazi wakili mmoja mashuhuri kumtetea mke wake mahakamani atakapomshtaki Coleen Rooney.

Baada ya Rebeccah kumtishia Coleen atamchukulia hatua za kisheria kwa kumchafulia jina, Coleen alimjibu kwa kumfahamisha yupo tayari kukabiliana nae mahakamani.

Wiki iliyopita, Coleen alimmwagia povu nzito Rebekah akimshutumu kuwa snichi aliyekuwa akitoa taarifa za maisha yake kwa vyombo vya habari.

Ishu hiyo ikazua gumzo kubwa kweli kweli na hata mademu wengine wa wachezaji wakajitokeza kumshutumu Rebecacah kwa kuwa na tabia hizo za kisnitchi na hutoa taarifa zao na kuzipa wanahabari wa udaku.

Baada ya kutishia kumshtaki Coleen, mume wake Jamie naye kajiongeza tena katika hili baada ya kumunfollow Rooney.

Safari hii Vardy ameamua kuipa kampuni kubwa yenye mawakili makini sana Uingereza Harbottle kazi ya kumshtaki Coleen wakitaka ashurutishwe kuwasilisha ushahidi alionao kuhusu madai yake dhidi ya mke wake.

Advertisement

Advertisement