Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe kina Man Dojo, Domokaya walipigwa!

Muktasari:

Sasa jamaa hao waliotamba na ngoma za Nikupe Nini, Wanoknok na Dingi zilizopo kwenye Albamu ya Taswira, walivuna mkwanja mbuzi tu unaambiwa.

UNAWAKUMBUKA Man Dojo na Domokaya? Ndio wale jamaa wa Arachuga ambao waliingia Bongo na kuwasha moto kinoma huko kwenye Bongo Fleva miaka ya 2003 hivi.

Sasa jamaa hao waliotamba na ngoma za Nikupe Nini, Wanoknok na Dingi zilizopo kwenye Albamu ya Taswira, walivuna mkwanja mbuzi tu unaambiwa.

Wasanii hawa ambao kwa sasa wameanza kurudi kwa kasi wamazungumza na Mwanaspoti na kufichua kwamba, kupitia mauzo ya albamu ya Taswira kila mmoja alivuna Sh 75 kwa kila mauzo ya kaseti moja.

Wamesema kuwa wakati wameachia albamu hiyo walianza kwa kugonga kopi 20,000 ambapo mgawo wao ulikuwa Sh 200 kwa kaseti moja, ambapo Sh 50 ilikwenda kwa uongozi na Sh 150 walipigana pasu kila mmoja akichukua Sh 75. Kwa mgawo huo kila mmoja aliondoka na Sh 1.5 milioni.

“Ndugu yangu tukizungumzia faida ya albamu ya Taswira, ukweli hatujapata faida kwani hatuwezi kusema kiasi gani tumeingiza kwani, hatujawahi kupata fedha taslim,” wamesema.