Kumbe ishu ya Shishi, Uchebe iko hivi buana

Sunday October 11 2020

 

By KELVIN KAGAMBO

Ebwana eeeh! Huko mjini Instagram vita ya mwanamuziki Shilole na aliyekuwa mume wake, fundi gereji maarufu Uchebe inaendelea. Uchebe akiposti pisi yake mpya, Shishi Baby anamposti jamaa aliyerithi mikoba ya Uchebe, mpaka kieleweke.

Moja ya picha aliyoiposti Shilole hivi karibuni ilikuwa ikimuonesha yeye na beibe wake mpya wakiwa vacation huku wakicheka kwa furaha. Kisha moja ya comment kutoka kwa shabiki ikasema: “Dah! Umeruka mkojo umekanyaga haja kubwa dada ‘angu, wewe ilitakiwa upate mtu mwenye miaka 35 au zaidi, kwa huyu uliyempata jiandae kulia tena.”

Shilole akaijibu comment hiyo kwamba: “Udogo wa mwili usikutishe, huyu ni babu.”

Ikumbukwe kabla ya Uchebe ambaye inatajwa alikuwa ni mdogo kiumri kwa Shishi Baby, Shilole pia alikuwa anatoka na mwanamuziki Nuh Mziwanda ambaye pia alikuwa ni mdogo kiumri kwake.

Ndoa ya Uchebe na Shilole imedumu kwa miaka miwili tu, walifunga Desemba 2017 na ilivunjika 2020 kwa madai ya kwamba mwanaume alikuwa amkifanyia vitendo vya kikatili mkewe ikiwemo kumpiga.

Advertisement