Ben Pol: Nakuja kwa kishindo cha Wapo

Wednesday June 12 2019

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam.Baada ya kimya kingi, mwanamuziki Ben Pol amekuja na wimbo mpya uitwaa Wapo.

Ben Pol alisema ukimya wake ulilenga kuandaa kishindo cha kuwapa wimbo mkali mashabiki wake amefanikiwa juu ya hilo.

Nyimbo yake hiyo inazungumzia suala mapenzi, jambo alilolieleza lina maisha halisi ya watu na anaamini ujumbe utakuwa mtamu kwao pindi wakiisikiliza nyimbo hiyo.

"Sikukaa bure nilikuwa nafanya vitu vingi vya kimuziki na ndio maana nimeachia kibao cha Wapo, mashabiki wangu wakisikiliza watapata burudani, elimu.

"Nakuja na kishindo kikubwa kwani kuna kolabo ambazo nimefanya na wasanii tofauti tofauti, bado gemu la muziki wa aina ninaoufanya kwangu upo wazi kwa maana ninavionjo vyangu tofauti na wengine," alisema Ben Pol.

Advertisement