Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tandahimba yaanzisha mashindano ya soka

Tandahimba. Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imeanzisha mashindano ya soka kwa lengo la kuibua vipaji kwa kauli mbiu ya kupinga mimba za shuleni.

Mkuu wa wilaya, Sebastiani Waryuba alisema mashindano hayo ni fursa kwa vijana wenye vipaji, lakini hawajulikani.

Alisema kutakuwa na vituo tisa katika wilaya hiyo na wanaolengwa ni vijana wenyewe miaka 17 hadi 25 na wasiokuwa wanafunzi.

“Tumeona kama wilaya tutumie nafasi hii ili kuibua vipaji kwa vijana ambao hawasomi au walishamaliza shule na hawajapata nafasi ya kuonekana, lengo ni kuwatangaza vipaji vya Wanatandahimba wenye vipaji tuwaibue na kuwatangaza ili kuonyesha vipaji, hatutarajii wanafunzi kushiriki kwa sababu shuleni wanao utaratibu wa kuibua vipaji,” alisema Waryuba.

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Tandahimba, Hamis Kangomba alisema wilaya hiyo ina vijana wenye vipaji hawajulikani, lakini kuanzishwa kwa mashindano hayo ni fursa kwao.

Alisema kauli mbiu ya mashindano hayo ni kupunguza mimba za utotoni ambazo ni changamoto.

Mchezaji Yasin Hamis alisema mashindano hayo yatawasaidia kuwa sehemu ya ajira kama jamii na wadau wa maendeleo watawaunga mkono.

“Mpira kwanza unaifanya afya kuwa imara mbali na burudani pia ni ajira kama ukipewa kipaumbele kwa sababu kila siku tunawaona wapo vijana waliofanikiwa kimaisha kutokana na mpira kama ilivyo kwa Mbwana Samatta ambaye anapeperusha bendera ya Tanzania Ulaya, hivyo na sisi Tandahimba tukipewa sapoti tunaweza,” alisema Hamis.