Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta:Wanahitajika maproo wengi Stars

Muktasari:

  • Samatta anasema mchezaji anayecheza nje,anakuwa amejifunza vitu tofauti vinavyokuwa vinaibeba Taifa Stars,inapokuwa na majukumu ya kimataifa.

STAA wa kimataifa anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Genk,Ubeligiji amesema kuna haja chipukizi wanaocheza ligi ya VPL, kuangalia soka la nje,ili kupata uzoefu wa kulisaidia taifa.

Samatta anasema mchezaji anayecheza nje,anakuwa amejifunza vitu tofauti vinavyokuwa vinaibeba Taifa Stars,inapokuwa na majukumu ya kimataifa.

"Taifa Stars, inapendeza iwe na wachezaji zaidi ya sita ambao wanacheza nje ya nchi,wanakuwa wana mbinu mbalimbali za kuhakikisha hatua zinapatikana kama ilivyo kwa mataifa mengine,"anasema

Pia amezungumzia umuhimu wa mashabiki kwamba wanapokuwa wanajitokeza kwa wingi na kuwashangilia,inawapa hamasa ya kujua wanahitaji kuongeza bidii, ili kupata matokeo.

"Binafsi najua mashabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani,wanaposhangilia inatupa hamasa wachezaji kujua tunahitaji kupambana kwa watu ambao wapo nyuma yetu,"anasema.