Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichuya amshika pabaya Hans Poppe

HOFU imeanza kutanda pale Mitaa ya Msimbazi. Nyota Shiza Kichuya ambaye amepachika mabao saba mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara, mkataba wake utamaliza mwishoni mwa msimu na amesisitiza hatasaini mpya hadi huu wa sasa utakapomalizika.

Kwa uamuzi huo, Kichuya ameishika pabaya Kamati ya Usajili ya Simba inayoongozwa na Zacharia Hans Poppe na ametaka wajipange kikamilifu ili kumbakiza kwa mkataba mpya wa maslahi mazuri zaidi.

Kichuya ambaye sasa ameamua kuupiga mpira mwingi zaidi, amesema: “Malengo yangu ni hayo na nashukuru nakwenda vizuri, hata Stars mmeona nilivyohusika katika magoli yote matatu (dhidi ya Algeria, Stars ilipolala 4-1 na DR Congo, Stars iliposhinda 2-0) ambayo tumefunga katika mechi mbili na nimebaki na kibarua cha kuibeba Simba na kuisaidia kuchukua ubingwa.

“Yote haya nafanya kwa sababu natambua mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu huu ili kuwa na thamani na kupata pesa nyingi kwenye usajili ni kuonyesha uwezo zaidi.

“Naipa nafasi kubwa Simba kunibakiza, lakini kama kuna jingine litajulikana mwisho wa msimu.”

Dhidi ya Algeria, kona ya Kichuya ndio iliyozaa bao la Simon Msuva, pia alitoa asisti kwa Mbwana Samatta kwenye goli la kwanza dhidi ya DR Congo kabla ya kufunga la pili juzi Jumanne.

BOLASIE AMPELEKA ULAYA

Straika wa DR Congo, Yannick Bolasie, anayekipiga Everton ya Ligi Kuu England, amevutiwa na Kichuya na kusema akipata wakala wa kimataifa, anaweza kucheza Ulaya.

“Nimeona vitu vingi vinavyompa nafasi ya kucheza Ulaya. Kuna timu zinaweza kumchukua,” alisema.