Jux atamani kupata mtoto

Muktasari:
- Muimbaji huyo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee kwa muda sasa, amesema hivi karibuni atafanikisha suala hilo la kupata mtoto kwa kuwa alijiwejea malengo ya akifika umri wa miaka 28 hadi 30 atakuwa na mtoto.
Dar es Salaam. Mwanamuziki wa RnB Jux amesema anatamani kupata mtoto kulingana na umri wake kumruhusu.
Muimbaji huyo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee kwa muda sasa, amesema hivi karibuni atafanikisha suala hilo la kupata mtoto kwa kuwa alijiwejea malengo ya akifika umri wa miaka 28 hadi 30 atakuwa na mtoto.
“Sina mtoto lakini Mwenyenzi Mungu akipenda siwezi nikasema siku gani lakini hivi karibuni tu, Mwenyezi Mungu akinijalia nitakuwa na mtoto, kwani ni kitu nilichokuwa natamani sana kuwa nacho,” amesema.
“Sio kama nilikuwa sitaki kupata mtoto, bali mtu wa kuzaa nae, unazaa na nani? Na huyo mtu unayezaa naye yeye mwenyewe yupo vipi?, japo sometime huwa inatokea unampa ujauzito mwanamke ila inatakiwa kuwa makini sana,” amesema.
Hata hivyo Jux hakusema kama atazaa na mpenzi wake Vanessa au kuna mwanamke ambaye tayari ameshampa ujauzi kutokana na kauli yake ya hivi karibuni atapata mtoto.