Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

HAMASA-Robben na Ribery mihimili ya mataji huko Bayern

Muktasari:

Pia nilizungumza na mwandishi na mtunzi wa vitabu, Ronald Reng ambaye moja ya kitabu chake maarufu kinaitwa ‘Robert Enke: A Life too Short.’

KATIKA toleo lililopita kwenye kitabu cha Pep Confidential, mwandishi Marti Perarnau alianza mazungumzo yake na Ronald Reng, mtunzi maarufu wa vitabu ambaye aliwahi kuwa karibu na kocha Pep Guardiola wakati huo akiwa na klabu ya Barcelona. Sasa endelea…

Pia nilizungumza na mwandishi na mtunzi wa vitabu, Ronald Reng ambaye moja ya kitabu chake maarufu kinaitwa ‘Robert Enke: A Life too Short.’

Ronald aliishi Barcelona kwa miaka kadhaa na ameshuhudia Barca ya Pep kwa karibu na hivyo ana nafasi nzuri ya kuilinganisha timu hiyo na Bayern.

“Wachezaji wa Bayern wamenishangaza zaidi kuliko Pep mwenyewe, nilikuwa namfahamu Pep tangu akiwa Barca na nilikuwa nakijua fika kipaji chake katika ubunifu na namna alivyo mtu mwenye mawazo na kuja na mbinu mpya.

“Hata hivyo, uvumilivu ambao wachezaji wamekuwa nao katika kujifunza umenishangaza, kwa namna nyingine haya ni mabadiliko ya msingi ni kama vile wachezaji walikuwa wamehamia nchi ya ugenini ingawa bado kuna tofauti kubwa katika uchezaji wa Bayern na ule wa Barca. “Kuna zile mechi zisizo za kawaida au mechi za matukio ambazo kwa kawaida zinachezwa uwanja wa nyumbani, hapo unaweza kuona hali ile ile ya ushindani lakini mechi za aina hii ni chache.

“Bayern ina uwezo wa kukuadhibu kwa nguvu zote tangu mwanzo, Barca hawana uwezo huo ni ule uwezo wa kutengeneza kitu pale kinapokosekana,” anasema Ronald.

Pengine jambo la kufurahisha kwa Ronald katika tukio zima ni ukweli kwamba mwaka 2013 walishinda mataji matatu nab ado tukio hilo halikuwatoa katika njaa yao ya kusaka mafanikio.

“Kwanza ni muhimu kusema kwamba mabadiliko muhimu ya kocha yamekuwa na maana kwenye timu hata wakati wakisaka mataji matatu, hadi Januari wachezaji tayari walifahamu kwamba Pep ndiye atakayeteuliwa kuwa kocha na hilo lilikuwa na faida kwao kisaikolojia

“Kwa kufahamu au kutofahamu wengi wao walianza kumpa ushirikiano zaidi Heynckes (Jupp) kwa sababu alikuwa ni mtu ambaye anajiandaa kuondoka, hata kwa Jupp pia ilikuwa rahisi kuiongoza timu ya wachezaji ambao walivutiwa naye.

“Wachezaji kama Robben na Ribery ambao walikuwa mhimili wa mataji waliyopata hawakuwa wakijiangalia wao na tofauti zao binafsi, walikuwa wakimfikiria kocha wao ambaye alikuwa mbioni kuondoka. Kwa hiyo kimsingi nafasi ya Pep ilianza kuwapo kabla hata ya kuja hapa (Bayern).

“Na kwa sasa wanacheza katika kiwango cha juu, matokeo yao ni ya kuvutia lakini pia ni hivyo hivyo kwa namna ya uchezaji wao, aina ya uchezaji wao kwa sasa ni mgumu zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana, pasi zaidi, uchezaji wenye maana na mbinu nyingi, hakika ni ubunifu wa kiwango cha aina yake unaoonekana kwenye soka.

“Wachezaji hawa tayari washashinda kila kitu lakini bado wanavutiwa na hali ya kuwaambia rafiki zao, ‘Nachezea timu ya Pep Guardiola.’ Hili si jambo linalotokea mara kwa mara, naweza kukwambia hivyo, ukweli ni kuwa wachezaji ni wakosoaji wakubwa wa makocha wao, wanakuwa tayari kwa haraka kuangalia makosa, lakini hapa ni kinyume.

“Hapa kuna umakini shauku ya kutaka kujua kuhusu Pep, pia walishangazwa na aina ya mazoezi yaliyoanzishwa, ukweli ni kwamba ujio wa Pep umekuwa hamasa kubwa kwa timu hii, uvumbuzi mkubwa ulioonekana msimu huu, wakongwe wanaocheza katika kiwango chao nao wanaweza kubadilika katika kipindi kifupi,’’ anasema Ronald.

Februari ni mwezi wa Bayern kuangazia mambo, mtazamo wa kiwango kizuri cha uchezaji cha Januari si tu kuwa ulimaanisha ushindi na tofauti kubwa ya pointi katika ligi ya Bundesliga pia uliwawezesha kubadili mtazamo wao na kuanza kuifikiria Ligi ya Mabingwa jambo ambalo Pep alikuwa akitaka kuachana nalo hadi hapo watakapotwaa taji la Bundesliga.

Hata hivyo, hilo ni jambo lisiloepukika, na wachezaji hadi hapo akili zao zikawa huko, walipambana katika mazoezi yao huku wakidhihirisha shauku waliyokuwa nayo, tayari walishaonja utamu wa taji la ligi ya mabingwa na hawakutaka kuona utamu huo ukiwaponyoka mikononi mwao.