Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Mrema Yanga damu bwana

Muktasari:

  • Mwaka 1994 ulitokea mgogoro wa wanachama walitaka klabu iwe kampuni huku wafadhili wakipinga.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema amesema sababu kubwa iliyomfanya kuishabikia Yanga ni baada ya kufanikisha kusuruhisha mgogoro wa timu hiyo uliodumu kwa muda mrefu.


Mwaka 1994 ulitokea mgogoro wa wanachama walitaka klabu iwe kampuni huku wafadhili wakipinga.


Mremba aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu alisema kitendo cha kujiingiza katika mgogoro wa timu hiyo na kufanikisha kuuzima kilimpa hamasa kubwa na kujikuta akiishabikia.


“Mimi ni nani hata nisiishabikie Yanga bwana,  siunaona hata timu yenyewe inavyofanya vizuri sasa, niliwasaidia kulikuwa na mgogoro, lakini kwa ujasiri niliyokuwa nao niliweza kusuruhisha,” alisisitiza.


Mrema alisema mgogoro huo ulimpa umaarufu mkubwa; “kipindi kile mimi nilikuwa waziri nisiyekuwa na wizara maalumu hivyo niliweza kupenya kila sehemu kuhakikisha mgogoro ule unaisha na kweli mambo yalikuwa mazuri kwa upande wangu mpaka leo ndiyo timu ninayoipenda hasaa,”aliongeza Mrema.


Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema muda mwingi amekuwa akitumia kuishangilia timu hiyo yenye makao yake makuu Mtaa Jangwani na kwamba anamiini ndiyo timu bora kwa sasa ukilinganisha na nyingine.