Yanga yaanza kunoa makali kwa ushindi wa mabao 10-1 Moro

Monday July 15 2019

 

By Khatimu Naheka

Dar es Salaam. Yanga imeanza kwa kishindo mechi zake za kirafiki baada ya kushinda mabao 10-1 dhidi ya Academic ya Tanzanite ya Mkoani Morogoro.

Katika mchezo shujaa amekuwa winga mkongwe Mrisho Ngassa aliyefunga mabao matatu pekee yake.

Wachezaji wapya waliofanikiwa kufunga mabao katika mchezo huo ni  winga wa kushoto Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Juma Balinya ambao ni wachezaji wa kigeni huku kiungo Mapinduzi Balama naye alifanikiwa kucheka na nyavu wote wakifunga bao moja kila mmoja.

Wafungaji wengine ni pamoja na Raphael Daudi, Papy Tshishimbi, Feisal Salum 'Fei Toto, ambao nao wakifunga bao moja kila mmoja.

Mshambuliaji mpya Mzambia Maybin Kalengo hakufanikiwa kucheza mchezo huo kufuatia kupata maumivu ya kifundo cha mguu kwenye mazoezi ya jana jioni.

Mchezo huo ulikuwa maalum kwa lengo la kupima mazoezi ya stamina yaliyofanyika kwa wiki moja tangu kuanza kwa kambi hiyo.

Advertisement

Advertisement