Waziri wa Michezo Cameroon amtimua kocha Seedorf

Tuesday July 16 2019

 

Yaoundé, Cameroon. Kocha wa Cameroon, Clarence Seedorf anakuwa kocha wa tano (5) kutupiwa virago baada ya kushindwa kuisaidia timu yake kufanya vizuri katika fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2019.

Seedorf ameonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kushuhudia mabingwa watetezi wakitolewa katika robo fainali ya mashindano hayo.

Waziri wa michezo wa Cameroon, Narcisse Mouelle Kombia alitangaza katika televisheni ya taifa kuwa Seedorf anatakiwa kuacha kazi ‘haraka iwezekanavyo’ kwa sababu si mtu sahihi wa kuiongoza Indomitable Lions”.

Kombi amemtuhumu Seedorf “kwa kushindwa kuiongoza timu” amekuwa na matatizo ya msaidizi wake Patrick Kluivert ambaye tangu amechukua jukumu hilo alikuwa akitaka kupewa jukumu la kuwa kocha mkuu na siyo msaidizi.

Makocha wengine waliopoteza vibarua vyao ni pamoja na Emmanuel Amunike (Tanzania), Sebastien Desabre (Uganda), Javier Onaindia Aguirre (Misri) na Paul Put wa Guinea.

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Guinea, limemtimua kazi kocha wake mkuu Paul Put (61) pamoja na benchi lote la ufundi.

Advertisement

Advertisement