Uamuzi kesi ya Aveva, Kaburu waahirishwa

Muktasari:


Katika rufaa hiyo DPP, anapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea Aveva na Kaburu mashtaka ya utakatishaji fedha na kuwapa masharti ya dhamana.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema hakimu anayeendesha kesi  inayomkabili aliyekuwa Rais wa klubu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange amepata hudhuru.

Wakili wa Serikali Mkuu Shedrack Kimaro alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally  kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya maamuzi na wapo tayari kusikiliza.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) aliwasilisha maombi ya kutaka Mahakama hiyo isitishe usikilizwaji wa shauri hilo.

Septemba 20, 2019 DPP aliwasilisha ombi hilo kutokana kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Katika rufaa hiyo DPP, anapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea Aveva na Kaburu mashtaka ya utakatishaji fedha na kuwapa masharti ya dhamana.

Hakimu Ally alisema Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeendesha kesi hii amepata udhuru hivyo anaihairisha shauri hilo kwa siku nyingine.

"Nimekuja leo (Ijumaa) baada ya hakimu anayeendesha shauri hili kupata dharula nitaliahirisha hadi siku nyingine," alisema Ally.

Ally aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 5 mwaka huu litakuja kwa ajili ya maamuzi.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwaa na mashitaka tisa ambapo Septemba 19 mahakama hiyo iliwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji fedha kwakuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuyathibitisha.

Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila watakaosaini bondi ya Sh 30 kila mmoja.

Hata hivyo, Mahakama hiyo iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashitaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha.