Tanasha arudi kwa 'Diamond' kimtindo

Wednesday June 3 2020

 

By ELIYA SOLOMON

LICHA ya kuhusishwa na mgogoro wa kimapenzi, mzazi mwenzie, msanii Diamond Platnumz, mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna ameonyesha kuwa hana hiana, baada ya kurekodi video ya binamu  wake akicheza wimbo wa 'Quarantine' wa msanii huyo.

Tanasha 24, ndiye aliyehusika kurekodi video hiyo huku  binamu wake huyo ambaye ni mtoto wa kike akiwa amesimama juu ya meza na Tanasha akiwa anafuatisha wimbo huo kwa kuuimba.

Baada ya msanii Diamond kuiona video hiyo, aliiposti kwenye 'Instagram story' na kumshukuru Tanasha kwa upendo wake alioonyesha licha ya tofauti wanazohusishwa nazo

"Asante sana Tanasha Donna kwa video yako" aliandika Diamond.

Tanasha ni miongoni mwa wanawake ambao wamewahi kuwa na uhusiano na Diamond na kupewa sapoti ya kutosha kwenye masuala ya muziki.

Ikumbukwe waliimba pamoja wimbo wa Gere uliotoka miezi kadhaa iliyopo.

Advertisement

Mbali na Tanasha kuhusika kwenye wimbo wa Quarantine, Zari pia alionekana siku chache zilizopita akiucheza wimbo huo akiwa na mtoto wake, aitwaye Tifah aliyezaa na Diamond.

Baada ya kuiposti video hiyo, dakika chache aliifuta kwa kuhofia pengine baadhi ya mashabiki wangeweza kumchukulia tofauti kuhusiana na video hiyo.


Advertisement