Stars yapasuka jioni

Muktasari:

TAIFA Stars ikicheza kwa mara ya kwanza tangu janga la corona lililpoibuka Machi mwaka huu, jioni hii imepauka nyumbani baada ya kunyukwa bao 1-0 na Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, huku ikishuhudia kiungo Jonas Mkude akitolewa kwa kandi nyekundu kipindi cha pili.

TAIFA Stars ikicheza kwa mara ya kwanza tangu janga la corona lililpoibuka Machi mwaka huu, jioni hii imepauka nyumbani baada ya kunyukwa bao 1-0 na Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, huku ikishuhudia kiungo Jonas Mkude akitolewa kwa kandi nyekundu kipindi cha pili.
Mechi hiyo iliyokuwa tamu, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam ilitibuliwa na eneo la kuchezea (pitch) kutokuwa kwenye ubora wake, ilipokea kipigo hicho cha sita kutoka kwa wapinzani wao hao katika mechi 21 walizokutana tangu mwaka 1971. Katika mechi zao 21, Tanzania imewatambia Warundi mara 12 na mechi tatu ziliisha kwa sare.

Mchezo ulivyokuwa
Katika kipindi cha kwanza kilimalizika huku kukiwa hakuna timu yoyote ambayo imeona goli la mwenzake.
Stars dakika 5 walifanya shambulizi kupitia kwa Idd Seleman 'Nado' aliyepigiwa pasi na Feisal Salum na yeye kupiga shuti lililopita juu kidogo ya goli.
Katika kipindi cha dakika 15 za kwanza Stars walikuwa wanatumia mawinga Simon Msuva na Idd Seleman kupeleka mashambulizi
Mawinga hao walikuwa wanatumia mbinu ya kubadilishana kushoto na kulia ili kuweza kupeleka presha langoni kwa Burundi na walikuwa wanafanikiwa.
Dakika 15 Stars ikosa bao kupitia nahodha wake, Mbwana Samatta, baada ya kuonganisha kwa kichwa krosi ya Shomari Kapombe na mpira kutoka kwa juu.
Refa Martin Saanya alitoa kioja dakika 22 baada ya kumsukuma mara mbali mshambuliaji, Mbwana Samatta baada ya mchezaji huyo kufanyiwa madhambi lakini muamuzi huyo ahakuonyesha ishara ya faulo na ndipo Samatta ambaye ni nahodha alimfata lakini aliambulia kusukumizwa.
Washambuliaji wa Burundi wakiongozwa na Saido Berahino walikuwa wanashindwa kupenya safu ya ulinzi ya Stars ambayo ilikuwa inaongozwa na Bakari Mwamnyeto na Abdallah Kheri.
Dakika 34 beki Emery Nimubona alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi winga wa Stars, Idd Seleman ambaye alimtoka beki huyo kwa spidi na kuvutwa shati.
Dakika 39, kiungo wa Burundi, Steve Nzigamasabo baada ya kumfanyia madhambi Feisal Salum.
Viungo wa Stars, Jonas Mkude na Said Ndemla walikuwa wanakaba hukunwakimuacha Feisal Salum atawale uwanja kwa kucheza zaidi.
Stars walionekana kupunguza spidi kuanzia dakika 40 na kuanza kuwapa uhuru washambuliaji wa Burundi nafasi ya kuanza kulisogelea lango la Stars.
Dakika 45+ kiungo wa Stars, Jonas Mkude alionyeshewa kadi ya njano baada kuunawa mpira nje ya boksi la Stars na kuwa faulo ambayo haina madhara.

Samatta chini ya ulinzi
Mshambuliaji Mbwana Samatta wa Tanzania amejikutabakiwa chini ya ulinzi wa kutosha kutoka kwa mabeki wa Burundi, Fredrick Nsabiyumva na Erick Ndizeye.
Mabeki hawa walikuwa wanatumia miili yao mikubwa katika kupambana na Samatta, walikuwa wanafanikiwa kutokana na urefu na maumbo makubwa waliyonayo.
Dakika 33 Samatta alipigiwa pasi na Feisal Salum iliyopenya moja kwa moja ndani ya boksi lakini ya boksi lakini alikutana na kigingi.
Katika kipindi cha pili timu zite ziliingia zikionyesha kuhitaji bao la kuongoza ili amtangulie mwenzake.
Stars ilikaribia kuandika bao kupitia kwa Simon Msuva baada ya kupigiwa pasi ndefu na Idd seleman na yeye kuutuliza kifuani na kuwazidi spidi mabeki wa Burundi na kuupiga mpira ukaenda kugonga mwamba lakini kipa Onesime Rukundo aliudaka mpira huo.
Stars ilifanya mabadiliko dakika 59 katika safu ya kiungo kwa kumtoa, Said Ndemla na kuingia Salum Abubakar, Idd Seleman na kuingia Ditram Nchimbi, huku upande wa Burundi wakiwatoa Steve Nzigamasabo na Mohamed Amissi na kuingia Blaise Bigirimana na Cedrick Urasenga.
Kiungo wa Burundi, Ndayishimiye Youssuf alionyeshewa kadi ya njano baada ya kuigiza kama ameumia dakika 69.
Stars walionekana kukata upepo, hali ambayo iliwafanya Burundi wafunguke zaidi kuanzia dakika 60.
Kocha wa Burundi, Ndayizeye Jimmy alionyesha kuhitaji bao baada ya kufanya mabadiliko dakika 72 kwa kumtoa nahodha wake, Saido Berahino na kuingia Bonfils Bimenyimana ili kwenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.
Dakika chache baadaye kiungo Jonas Mkude alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na nyekundu akitolewa nje baada ya kufanyiana fujo na Said Ntigamasabo, wakati huo huo kocha Etienne  Ndayiragije alifanya mabadiliko ya kumtoa Mbwana Samatta na kuingia Ally Msengi.
Burundi walipata bao pekee dakika 85 baada ya mshambuliaji wao Said Ntizansabo kufyatuka shuti kali na kwenda moja kwa moja wavuni.
Baada ya bao hilo Stars ilifanya mabadiliko ya kumtoa Feisal Salum na kuingia Mzamiru Yassin, mbinu za kocha Ndayiragije zilikuwa zinaonekana katika kuzuia.
hadi dakika 90 zilipomalizika matokeo yalikuwa 1-0 kwa Burundi na Simon Msuva alikiri walizidiwa na wenzao kwa kushindwa kutumia nafasi walizopata na kwa kuwa ni mchezo wa maandalizi ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya Tunisia anaamini Kocha wao atarekebisha makosa kabla ya mechi ya ugenini.
Upande wa Berahimo alikiri mechi ilikuwa nzuri na yenye ushindani na wanafurahi kushinda mchezo huo wa ugenini, kwani kilikuwa kipimo tosha kwao kuelekea kwenye mechi zao za kimataifa za michuano ya kuwania Fainali za Afcon 2021.

Vikosi vilivyoanza:
Tanzania:David Kissu, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdallah Kheri, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude, Said Hamis, Feisal Salum, Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Idd Seleman.


Burundi: Onesime Rukundo, Eric Ndizeye, Fredrick Nsabiyumva, Said Ntigamasabo, Philip Nzeyimana, Nimuboma Emery, Ndayishimiye Youssuf, Stev Nzigamasabo, Saido Berahino, Cedric Amissi na Mohamed Amissi.