Samatta abaki Ligi kuu England, Villa ikitoa sare

Sunday July 26 2020

 

Timu ya Aston Villa ya England imefanikiwa kupigana vita ya kushuka daraja kwa mafanikio wakisalia katika ligi hiyo kufuiatia matokeo ya sare ya bao 1-1 huku waliokuwa wahindani wao katika vita huyo Watford ikiterema ligi hiyo.
Villa ikiwa ugenini mbele ya West Ham ndio waliotangulia kupata bao kipindi cha pili dakika ya 84 likifungwa na kiungo Jack Grealish akimalizia pasi ya John McGinn.
Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika moja pekee kwani wenyeji walisazisha dakika ya 85 shukrani kwa bao la Andriy Yermolenko akimalizia pasi ya Declan Rice na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare hiyo.
Samatta ambaye alicheza mchezo huo kwa dakika 68 kabla ya kutolewa nafasi yake ikichukuliwa an Keinan Davis aliambulia kadi ya njano  dakika ya 41 huku akifanikiwa kubakia rasmi katika ligi hiyo.

Samatta ambaye alicheza mchezo huo kwa dakika 68 kabla ya kutolewa nafasi yake ikichukuliwa an Keinan Davis aliambulia kadi ya njano  dakika ya 41 huku akifanikiwa kubakia rasmi katika ligi hiyo.
Matokeo hayo sasa yanaifanya  Villa kumaliza ligi katika nafasi ya 17 wakifikisha pointi 35 kazishuhudia Watford waliokubali kipigo cha mabao 3-2 mbele ya Arsenal wakiteremka rasmi sambamba na AFC Bournemouth na Norwich City.

Advertisement