Pochettino amtega Eriksen

Saturday August 17 2019

 

By Thomas Ng'itu

KOCHA Mkuu wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino ameweka wazi wanaweza kumkosa mchezaji wake Christian Eriksen ndani ya mwezi huu.
Spurs wamemuekea Eriksen ofa mpya ya mshahara pauni 200,000 kwa wiki lakini kiungo huyo ameweka wazi bado hayupo tayari kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.
Pochettino alisema alisema lolote linaweza kutokea kwasababu sio yeye ambaye anataka liwe, lakini muda mwingine lazima mambo yafanyike.
"Bado tunatakiwa kusubili mpaka Septemba 22, hakutakuwa na mabadiliko makubwa ambayo yataleta matatizo kwetu, tunaweza kubadilisha mawazo na mchezaji akabadilisha mawazo yake, kwa muda huu ni ngumu kusema moja kwa moja tusubili Septemba ifike,"alisema.
Aliongeza timu yake bado haijatulia kama ambavyo anataka iwe, lakini bado anafanyia kazi ili kuhakikisha suala hilo linakamilika inapofika Septemba 2.
"Nataka kuwa na timu ambayo imetulia, lazima nikae chini na wachezaji wangu na kuzungumza nao kwa mapana na kuweka misingi yangu, naamini nitafanikiwa katika hili," alisema.

Advertisement