Harmonize afungua mwaka 2020 na wimbo Hainistui

Friday January 3 2020

Mwanaspoti-tanzania-Harmonize-Diamond-afungua -mwaka 2020-Hainistui-muziki

 

Dar es Salaam. ‘Usiruhusu dharau, kejeli, matusi, kukatishwa tamaa,  vitisho na  masimango...Hiyo ni mistari iliyoandikwa na Harmonize chini ya picha ya mtu anasoma gazeti ikiwa ni picha ya wimbo wake mpya ‘Hainistui’.

Katika picha hiyo inayomuonyesha mtu anasoma gazeti, ukurasa wa kushoto mwaka gazeti hilo kumeandika mojawapo ya shairi linalopatikana katika wimbo wake huyo mpya, yakisomeka...Wenzako watakuroga au nawe usharoga maana hunaga woga...

Maelezo chini ya picha hiyo yaliendelea...Najua upo kazini ..!! Wenda miangaikoni kutafuta riziki ...!!! Pengine wenda umekaa tuu kijiweni ..!!! Kichwani una ndoto Kibao ambazo unataka kuzitimiza naomba nikuambie maneno haya machache yafuatayo...!!! Usiruhusu dharau, kejeli, matusi, kukatishwa tamaa vitisho na masimango vikazisimamisha ndoto zako amini kwamba hata huyo anaekutisha kesho yake mwenyewe haijuwi.

Harmonize ameendelea kuwapa usia aliowadhamiria kwa kuandika ...Mpangaji na mtoaji wa yote ni Mungu kama anayekutisha anajivunia utajiri basi utajiri ni wa Mungu,  kama akijivunia upeo basi anayetoa pia ni Mungu.

Ameandika... Kuanzia sasa All I need ni wewe kutostuka na mafanikio au maneno ya mtu yeyote mana ukiwa unajali sanaa...!! mwenzio kapata nini au kafanya nini hapo ndipo uchawi unaanziaga....!!!!! Mind your own business Let's Go 2020...

Advertisement