VIDEO: Wachezaji wa Simba wazomewa bandarini Dar es Salaam

Tuesday January 14 2020

Mwanaspoti-Wachezaji-Simba SC-Mwanasport-Michezo-wazomewa-bandarini-Dar es Salaam

 

By THOMAS NG’ITU

Dar es Salaam. Baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar, kikosi cha Simba imepokewa kwa kuzomewa na mashabiki wake wakati wanawasili katika bandari ya Dar es Salaam wakitokea Zanzibar.

Baada ya kuwasili bandarini hapo mashabiki Simba na watu wengine waliokuwepo eneo hilo walianza kuwazomea wachezaji hao wakati wanatoka.

Wachezaji na benchi la ufundi walikuwa na nyuso za hasira kwa kitendo cha kuzomewa na mashabiki hao, lakini hawakuweza kujibu lolote zaidi ya kunyamaza na kuondoka kwa haraka katike eneo hilo.

Wachezaji hao pamoja na benchi la ufundi hawakuwa tayari kuzungumza badala yake kila mmoja alipanda usafiri wake kwenda makwao na wengine waliondoka na gari la timu.

Simba inatarajia kuondoka usiku wa leo kwa ndege kwenda mkoani Mwanza kwaajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu kesho Jumatano dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Advertisement