#KariakooDabi: Kagere amtumia salamu Yondani

Thursday January 2 2020

Mwanaspoti-Kagere- Simba SC-amtumia salamu-Yondani-Yanga- Tanzania-Watani wa Jadi

 

By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Wakati Simba ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa watani wa jadi Jumamosi, Meddie Kagere amesema hakuna beki anayemhofia Yanga.
Kagere aliyefunga mabao tisa katika Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema anatambua uwezo wa mabeki bora nchini wakiwemo wa Yanga, lakini hana hofu nao kwa kuwa anajiamini..
“Dabi huwa tofauti na michezo mingine ya kawaida natarajia itakuwa mechi ngumu  kwasababu kila timu itataka kushinda, lakini hakuna beki ninayemuogop najiamini naweza kufunga mbele ya beki yeyote,” alisema Kagere.
Kagere alifunga bao la ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa mwisho ambao Simba iliishinda 1-0 Februari 16, 2019.
Wakati huo huo, nahodha wa timu ya wanawake ya Simba  ‘Simba Queens’, Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’ alisema Yanga wanatakiwa kuwa makini na mshambuliaji huyo kutokana na ubora wake ndani ya eneo la hatari la wapinzani.
“Kagere ni mtafutaji muda wowote anaweza kuleta madhara. Kwa mtazamo wangu  mechi itakuwa ngumu Yanga ina wachezaji wazoefu kama Kelvin Yondani,” alisema Mwanahamisi.
Kagere na Yondani watakuwa kivutio katika mchezo huo kutokana na ubora na uzoefu wao katika mechi kubwa ikiwemo ya watani wa jadi ambayo Simba itakuwa mwenyeji Jumamosi.

Advertisement