Dida anarudi kivingine Ligi Kuu Tanzania Bara

Tuesday December 10 2019

Mwanaspoti-Dida-anarudi-Tanzania-Simba-Yanga-kivingine-Ligi-Kuu-Tanzania Bara

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Kipa Deogratius Munishi 'Dida' anatarajia kurejea kwa nguvu katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukaa nje kwa nusu msimu, tangu alipochwa na Simba.

Dida ameliambia Mwanaspoti kwamba soka ni kazi yake hivyo aliendelea na programu ya mazoezi licha ya kukaa nje kwa muda mwingi.

Kwa sasa anafanya mazoezi na timu ya taifa ya beach soka, lengo ikiwa nikujiweka fiti.

Dida alisema tayari kuna timu ambazo anaendelea kuzungumza nazo kwa ajili ya kusajiliwa dirisha dogo na kwamba itakayokuwa na dau kubwa basi atakubali kuvaa uzi wake.

"Siwezi kuzitaja kwa sasa kwa sababu sijafikia nazo makubaliano ili ninarejea uwanjani, nimejipanga na nipo fiti kwa ajili ya kufanya kazi,"alisema.

Alipoulizwa anaonaje nafasi yake ya kurejea klabu ambazo amewahi kuzitumikia hasa Simba na Yanga? Alijibu kuwa "Nina nafasi kubwa tu, kikubwa ni makubaliano na maslahi, sijaona cha kunizuia nisicheze timu hizo."

Advertisement

Advertisement