VIDEO: Wakazi afunika vibaya Tamasha Sauti za Busara Zanzibar

Sunday February 16 2020

Mwanaspoti, Wakazi afunika, Tamasha Sauti, Busara Zanzibar, Mwanasport, Tanzania

 

By RHOBI CHACHA

Zanzibar.Mwanamuziki wa hiphop nchini Tanzania, Wakazi amelitendea haki jukwaa la Tamasha Sauti za Busara 2020, baada ya kuimba muziki kwa kutumia vyombo na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria.

Wakazi alikuwa msanii wa tatu kupanda kutimbuiza katika tamasha hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo, Februari 16, katika ukumbi wa Ngome Kongwe.

Wakazi alipanda jukwaani baada ya kutanguliwa na bendi ya Siti kutoka Visiwani Zanzibar na msanii Mannyok kutoka Mauritius.

Wakazi amekuwa mmoja wa mabalozi wazuri wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, kamwe haachi utamaduni wake wa kuchanganya kiswashili na kiingereza katika mashairi yake yenye ujanja wa kucheza na maneno, misemo na nahau.

Wakazi ana kandamseto saba ameshazitoa rasmi pamoja na uteuzi wa tuzo ya Kora Award pamoja na Tiznee Award za kandamseto ya mwaka 2017 na Albami bora ya Hiphop mwaka 2018.

Advertisement