Siti Amina aliachika kwa mume wake sababu ya muziki

Muktasari:

Ikiwa Siti Omary ni kiongozi wa Siti & the band anasema, wanatumia elimu, talanta na ubunifu kuandaa muziki kutokana na maisha binafsi.

Zanzibar. Siti Amina ni kiongozi wa bendi ya The Siti iliyoko Zanzibar inayoshiriki tamasha la sauti za busara amesema aliachwa na mume wake kwa sababu ya kupenda kufanya muziki.

Mwanamuziki Siti Amina jina lake halisi ni Amina Omary amesema katika muziki amepitia changamoto nyingi ikiwemo kuachana na mume wake wa ndoa sababu ya muziki.

“Naongea kwa uchungu nikikumbuka muziki ulivyonitenganisha na aliyekuwa mume wangu, nimeachana nikiwa na mtoto mmoja wa kiume aitwaye Shabani toka mwaka 2012, kwa sababu alikuwa hataki nifanye muziki,

“Alikuwa ananipiga kila wakati nikipanda jukwaani kuimba, na hii yote alisikiliza maneno ya watu amabo ni rafiki zake walimwambia nimejiingiza kwenye muziki hivyo hatakuwa mke wake tena mimi  kwani muziki una mambo ya kihuni,” alisema Siti.

Siti anasema kwa sasa yuko ‘Single mama’ kwani hataki kuolewa wala kuishi na mwanaume ndani ya nyumba kwa kile akikumbuka matukio aliyopitia akiwa na mume wake.

“Nimeichukia ndoa kwa kweli, nimeteseka na ndoa yangu, hadi kuamua kuwa singo basi ujue nimepitia mengi ambayo mengine siwezi kuyasema, sitaki kuishi na mwanaume ndani kwa sasa, ila kwa wale wanaume wa hapa na pale wapo nao huwa nafanya kwa wakati na kuachana nao hapo hapo”

Siti watu wengi wanadhani ni Mzanzibar, kumbe ametokea Tanga kwa baba na  mama Mzaramo, amesema changamoto nyingine aliyopata kwenye muziki ni kununiwa na majirani na watu wake wa karibu  baada ya kumuona anafanikiwa katika muziki anaoufanya.

“Changamoto nyingine iliyoniumiza kupitia muziki sikukata tamaa japo sikuwa na raha, ni baada ya kununiwa na majirani na watu wangu wa karibu baada ya kuona nimeanza kupata mafanikio katika muziki, yaani walikuwa hawaniongeleshi kabisa hadi nikawa najiuliza ni mitihani gani Mungu ananipa, ila nilizidi kumuomba Mungu kila kulicha hali hiyo ipite”

 

MAFANIKIO ALIYOPATA KWENYE MUZIKI

Siti Omari anasema amejikuta anapenda muziki na kuamua kwenda kuusomea chuo cha muziki Zanzibar Dsma miaka mitatu kilichopo Mizingani.

Anasema faida aliyopata kwenye muziki hadi sasa ni kwamba muziki  umekuwa  kama kazi na kujielewa zaidi kama mwanamuziki pamoja na kutangaza nchi yake duniani.

Anasema hawezi kusema amefanikiwa kupata gari au kujenga nyumba sababu maisha yanaendesha  familia inategemtegemea hiyo ni moja ya mafanikio kupitia kazi yake.

Aidha anasema alitoa pesa katika shoo anazofanya kupitia muziki na kununua chombo cha muziki kinachoitwa Udi kipo kama gitaa.

ATOA OMBI KWA SAUTI ZA BUSARA

Siti kila mwaka anatumbuiza Tamasha la sauti za busara anasema imesaidia bendi yao kufungua milango pande za  Afrika na kuwapa nguvu wanawake wa Zanzibar,  anaomba  tamasha hili  lifanyike  mara tatu kwa mwaka hii ingesaidia kwa wasanii na wakazi wa Zanzibar.

AZUNGUMZIA THE SITI BAND

Ikiwa Siti Omary ni kiongozi wa Siti & the band anasema, wanatumia elimu, talanta na ubunifu kuandaa muziki kutokana na maisha binafsi.

Muziki huo wenye mahadhi ya taarabu umechanganyika mila nandesturi za kiarabu, kihindi, Uajemi na kiafrika Siti & the band wanachanganya aina hizo za muziki kutoka kwenye Jazz  kwenda kwenye regge na aina nyingine.

Anasema mbali na muziki huo kukosa promo hapa nchini lakini Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa muziki wa asili katika ukanda wa Esta Afrika.

“Katika kukuza muziki huu kundi la Siti band, limeanza kufanya kolabo na wasanii wakubwa nje ilikukuza muziki huu kupata nafasi katika sehemu mbalimbali.”

Anasema mpaka sasa bendi hiyo imetoa albam moja ikiwa ni njia ya kukuza muziki na kufanya dhiara nje ya nchi ambapo kwa mwaka wa jana wametembelea nchi sita za Afrika.

Anaendelea kwa kusema kuwa wanatamani kualikwa katika matamasha makubwa hapa nchin Wasafi festival, Feasta na Muziki mnene lakini imekua ngumu kupata nafasi.

"Tuna tamani kupata mualiko katika haya matamasha makubwa Ila imekua ngumu kwa sababu tumejenga matabaka ya muziki kila watu wanaipa nafasi style yao," anasem Siti.

Kundi la Siti band linawasanii sita siri ya mafanikio katika kundi hili ni upendo na umoja kati yao.

"Makundi mengi ya muziki hayadumu kwa muda mrefu kwa kukosa upendo baina yao na kujitambua tunashukuru Siti bandi hili kwetu halina nafasi kila mmoja ana nafas ya kusikilizwa, kuchangia kwa namna yoyote katika kundi." anasema siti Omary