Mshindi wa Mchongo wa Mwanaspoti apewa chake

Friday August 23 2019

 

By Berdina Majinge, Iringa

MSHINDI wa droo ya sita ya Promosheni ya Shinda Mchongo na Mwanaspoti, Nsangalufu Mwakasumbula, mkazi wa Makambako Mkoani Njombe amekabidhiwa zawadi ya fedha taslimu Sh100,000.
Tangu kuanza kwa promosheni hiyo hii ni mara ya tano mshindi wa promosheni hiyo anatokea ukanda huo kwa kujishindia kiasi hicho cha fedha na kufanya ukandaa huu kuvuna Sh500,000.
Mwakasumbula amesema alianza  kucheza promosheni  hiyo tangu ianze na safari hii ndio mara yake ya kwanza kushinda na mzuka ulipanda kutokana na kuona waakzi wenzake wa Iringa wakishinda zawadi kupitia shindano hilo.
“Kwanza sikuwa na uhakika kama kweli nimeshinda kwa sababu nilikuwa nimehamaki baada ya kupigiwa simu, ndipo nilipoamini kuwa mashindano haya si ya utapeli wala hwana washindi wao ni promosheni ya washiriki wote,” alisema na kuongeza;
“Nimeshuhudia Barongo anashinda mara tatu mfululizo nami nikasema sikati tamaa ya kushiriki awali niliona labda wanampa tu lakini baada ya kushinda nimeamini mashindano yapo na watu wanapewa fedha zao.”
Anasema furaha aliyokuwa nayo baada ya kukabidhiwa fedha zake haipimiki kwa kuwa ilimthibitishia ukweli na uhakika wa mashindano hayo.
Akizungumza baada ya kumkabidhi mshindi huyo Meneja Mauzo wa Mwananchi Communications Ltd Mkoa wa Iringa, Noel Mlowe amewataka wasomaji na wadau wa mwanaspoti mkoani Iringa kuendelea kushiriki promosheni.
“Nawasihi wasomaji wa mwanaspoti kuendelea kushiriki Promosheni na kujishindia zawadi kama smatifon ,pesa taslimi,Bodaboda”

Advertisement