VIDEO: Morrison azomewa akiwaaga mashabiki Yanga, asusa kukaa benchi

Sunday July 12 2020

 

By Mwandishi Wetu

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amekumbana na zomea zomea ya mashabiki wa timu yake huku akisusa kukaa kwenye benchi baada ya kufanyiwa mabadiliko.

Morrison amekumbana na kadhia dakika ya 67 kipindi cha pili baada ya kufanyiwa mabadiliko na kocha Luc Eymael ambapo alimtoa nafasi yake ilichukuliwa na Patrick Sibomana.

Baada ya mabadiliko hayo, mashabiki wa Yanga walishangilia huku wengine wakizomea.

Baada ya Morrison kutoka uwanjani aliunganisha moja kwa moja kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, ingawa kamishina wa mchezo Kassim Mpanga alijaribu kumrudisha kwa kumzonga bila mafanikio.

Morrison alivutana na Kamisaa sekunde kadhaa, kabla ya kumuacha mchezaji huyo akiingia vyumbani huku baadhi ya mashabiki wa upande wa Yanga wakimrushia chupa za maji.

Mara baada ya kuwa anatoka kwenye lango la kuingilia mashabiki alionekana akiwaga mashabiki wa Yanga waliokuwa jukwaa la karibu.

Advertisement

Advertisement