Morocco ampania Bilo Mwanza Derby

Friday August 23 2019

 

By James Mlaga,Mwanza

PAZIA la Ligi Kuu Bara linafunguliwa rasmi kesho kwa michezo mitano, lakini mzuka ali onao Kocha Hemed Morocco wa Mbao FC watakaoumana na Alliance ni mkubwa, akitamba kuwa ni lazima awazime waspinzani wao wanaoonekwa na Athuman Bilal 'Bilo'.
Mbao yenye makazi yake Wilaya ya Ilemela, jijini hapa imefanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa Nyamagana kujiandaa na 'Mwanza Derby', huku akisema kuwa kwa maandalizi aliyoyafanya haoni cha kuwazuilia kuwanyoosha Alliance.
Akizungumza na MCL Digital , Morocco amesema wamejipanga vizuri kuelekea pambano hilo hivyo Mashabiki wao wategemee ushindi katika mchezo huo wa kwanza kwa msimu wa 2019/2020.
"Leo tumefanya mazoezi mepesi ya kujiweka sawa kwaajili ya mchezo wa kesho, tunatarajia tutafanya vizuri kwasababu tumejiandaa , Mashabiki waje kutusapoti nasi hatuta waangusha " amesema Kocha huyo.
Mbao itashuka dimbani kesho kucheza na Alliance FC huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya msimu uliopita ambapo katika mechi mbili za Ligi hiyo walishinda moja na nyingine kutoka sare katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Advertisement