Moro, Kabamba wazua jambo Yanga

Monday June 1 2020

 

By THOMAS NG'ITU

WACHEZAJI wa Yanga, Lamine Moro na Erick Kabamba leo wameshindwa kufanya mazoezi na wenzao leo katika uwanja wa chuo cha Sheria, Dar es Salaam.

Wachezaji hao licha ya kutokuwa katika miongoni mwa walioshiriki programu ya leo, walikuwa wamekaa nje wakiangalia kile ambacho kinafanywa na wenzao.

Baada ya mazoezi kuchanganya, Moro aliondoka na kumuacha Kabamba ambaye alikuwepo hadi mazoezi yalipomalizika.

 Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema sababu ya wachezaji hao kukaa nje ni ugonjwa.

"Waliumia juzi hawa mimi najua hivyo tu mengine anajua daktari, kwa hiyo tunasubili daktari aseme hali ilivyo," alisema.

Lamine Moro amekuwa na mchango mkubwa msimu huu akimudu vizuri nafasi ya beki wa kati katika kikosi hiko.

Advertisement

Advertisement