Molinga ashindwa kuwanyanua mashabiki Yanga

Muktasari:

Molinga alikosa umakini katika umaliziaji kwa kushindwa kutumia nafasi hiyo hivyo kuilazimu Yanga kwenda mapumziko ikilazimishwa sare ya bao 1-1.

Dar es Salaam.Mshambuliaji raia wa DR Congo, David Molinga ameshindwa kuwanyanyua mashabiki wa Yanga baada ya kupoteza nafasi ya wazi dakika ya 45 katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania unaoendelea.

Molinga alipaisha mpira wakati kipa wa Polisi akiwa ametoka golini akiwa kwenye nafasi ya kufunga baada ya kupigwa mpira wa krosi na mabeki wa Polisi kujichanganya.

Molinga alikosa umakini katika umaliziaji kwa kushindwa kutumia nafasi hiyo hivyo kuilazimu Yanga kwenda mapumziko ikilazimishwa sare ya bao 1-1.

Mashabiki wa Yanga wakiwa wamenyanyuka vitini wakitarajia kushangilia bao la pili na ghafla upepo ulibadirika na kushika vichwa kwa ishara ya kusikitika baada ya mshambuliaji huyo kupiga shuti la mguu wa kulia lililopaa juu na kutoka wakati tayari kipa wa Polisi Tanzania akiwa ametoka golini.

Hadi mapumziko, Yanga ilionekana kumiriki mpira kwa asilimia 52 wakati wapinzani wao wakimiriki mpira kwa asilimia 48.

Molinga amejiunga Yanga kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu huu akitokea AC Lega ya DR Congo hajafanikiwa kuipatia Yanga bao mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, ingawa kocha Mwinyi Zahera ambaye leo Alhamisi anashuhudia mchezo huo akiwa jukwaani akisisitiza mshambuliaji huo ana kiwango bora hivyo mashabiki wawe na subira.