Mapema tu Alliance chali mbele ya Mbao FC

Muktasari:

Mchezo huo ni wa kwanza katika ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,ambapo timu hizo za jijini Mwanza kila moja inahitaji ushindi ili kuanza vyema michuano hiyo.

Bao la mapema dakika ya 13 kupitia kwa Frank Paschal kwa njia ya faulo limeipeleka Mbao FC mapumziko ikiwa mbele dhidi ya majirani zao,Alliance FC.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ambao upo mapumziko kwa sasa katika dimba la Kirumba jijini hapa,Alliance wameonekana kushambulia zaidi lakini ishu ya ufungaji mabao imekuwa changamoto.
Mbao walionekana kulinda zaidi,huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza ambapo haikuwachukua dakika nyingi kuweza kupata bao hilo na kujipa matumaini ya kuendeleza rekodi kwa wapinzani wake.
Hata kila timu ilipambana kadri ya uwezo wake,ambapo katika vuta nikuvute,wachezaji Babilas Chitembe (Mbao FC) na Michael Chinedu wa Alliance walijikuta wakitembezewa kadi za njano kwa kuwachezea rafu wapinzani wao.
Pia Kocha wa Mbao Hemed Morocco alionekana kufanya mabadiliko mapema kwa kumtoa beki,Rajabu Rashid na kumwingiza Kauswa Manumbu dakika ya 33.