Lescott amwambia Grealish awakatae Man U

Saturday February 15 2020

Lescott amwambia Grealish awakatae Man U,Manchester City ,Old Trafford,Jack Grealish,Aston Villa ,

 

BIRMINGHAM, ENGLAND . JOLEON Lescott ameanza zengwe. Unajua alichomwambia Jack Grealish? Si unajua staa huyo wa Aston Villa anasakwa na Manchester United kwa nguvu zote, basi Lescott, aliyewahi kuichezea Manchester City alipomwambia ni kwamba asikubali kwenye Old Trafford kwa sababu timu hiyo si miongoni mwa zilizobora kwa sasa.
Man United ilimtaka Grealish tangu kwenye dirisha la Januari, lakini nahodha huyo wa Aston Villa hakutaka kuondoka Villa Park kwa sababu kuisaidia timu hiyo kukwepa kushuka daraja kwenye Ligi Kuu England.

Lakini, kwa sasa Man United imetangaza wazi kwamba itamfungia kazi mwisho wa msimu kabla ya kuibuka kwa Lescott akimwambia akaye kwenda kujiunga na timu hiyo kwa sababu sio timu bora kwa sasa.

Advertisement