Kocha Liverpool awatahadharisha Porto vita inaendelea, Spurs yaituliza Man City

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah akipambana na wachezaji wa FC Porto

Muktasari:

Hata hivyo Sergio Aguero alikosa penalti dakika ya 13 kipindi cha kwanza huku wachezaji wa kikosi hicho Aymeric Laporte na Riyad Mahrez wakilimwa kadi za njano kila mmoja.

Mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochwa jana Jumanne usiku, Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FC Porto huku Tottenham Hotspur ikiizamisha Manchester City bao 1-0.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Naby Keita 1-0 dakika ya 5 na Roberto Firmino akiweka msumari wa mwisho dakika ya 61.

Kocha wa  Liverpool, Jurgen Klopp baada ya mchezo huo alisema ushindi huo dhidii ya Porto sio mwisho wa vita kwani kikosi chake kinatakiwa kujipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano.

Kocha wa FC Porto, Sergio Conceicao alisema anaamni kikosi chake kilistahili kushinda licha ya kutundikwa mabao 2-0.

Katika mchezo mwingine wa robo fainali, Spurs waliibuka kidedea baada ya kuitandika Manchester City, bao ambalo lilifungwa na Heung-Min Son dakika ya 78.

Hata hivyo Sergio Aguero alikosa penalti dakika ya 13 kipindi cha kwanza huku wachezaji wa kikosi hicho Aymeric Laporte na Riyad Mahrez wakilimwa kadi za njano kila mmoja.