Klabu Hispania zarejea mazoezini, Hazard afurahia

Tuesday May 19 2020

 

By AFP

Madrid, Hispania. Klabu za Hispania zimeanza mazoezi ya makundi ya wachezaji 10, kwa mujibu wa mwongozo, wakati Ligi Kuu (La Liga) ikipiga hatua nyingine kuelekea kurejea uwanjani baada ya kusimamishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.
Barcelona ilithibitisha kuwa kikosi chake kilirejea mazoezini jana saa 1:30 asubuhi, huku ikichapisha picha katika akaunti ya Twitter ikionyesha wachezaji kadhaa, akiwemo Gerard Pique na Sergio Busquets wakishiriki.
Wachezaji wa Real Madrid pia walifanya mazoezi katika kituo chao cha mazoezi pembeni ya jiji la Madrid, wakati klabu hizo zikipiga hatua kuelekea kufanya mazoezi pamoja na kikosi kamili.
Mwongozo uliotolewa na serikali ya Hispania unaruhusu kuongeza vipindi vya mazoezi hata katika maeneo ambayo bado hayajakamilisha kuondoa masharti ya kudhibiti maambukizi.
Hiyo inamaanisha kuwa Real, Barcelona na Aletico Madrid wanaweaza kufanya mazoezi katika makundi ya wachezaji 10, licha ya miji yote miwili-- Madrid na Catalonia kuendelea kutokuwa katika hatua yoyote ya maendeleo ya kuondokana na ugonjwa huo baada ya kushambuliwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo.
Hispania ni moja ya nchi zilizoathiriwa sana na Covid-19, ikiwa na jumla ya vifo 27,650 vilivyoripotiwa hadi Jumapili na zaidi ya watu 231,000 kuambukizwa.
"Ni uamuzi wa wizara. Ilikuwa ni muhimu kwa timu zote kuweza kufanya mazoezii kwa namna moja," alisema Javier Tebas, rais wa La Liga, Jumapili.
Tebas alisisitiza nia ya La Liga kuamlizia raundi 11 zilizosalia msimu huu baada ya ligi kusimamishwa katikati ya Machi.
Alisema Juni 12 ni tarehe ambayo wanatumaini ligi itarejea uwanjani.
health authorities in Spain and the trajectory of the virus.
"Tunafanyia kazi ligi kurejea Juni 11/12 na tunataka kuwa tayari bila ya kujali tarehe," Tebas aliiambia Movistar TV.
"Ni mamlaka za afya ambazo zitasema tuanze lini.
"Ningependa hilo litokee mapema iwezekanavyo, lakini ukweli ni kwamba hatuna tarehe yetu. Lazima tusubiri ruhusa kutoka mamlaka ya afya."
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa Jumamosi, klabu za michezo za wachezaji wa kulipwa "zinaweza kufanya mazoezi kwa vipindi kamili" wakati  "zikitekeleza hatua za kujikinga na usafi".
Taarifa hiyo iliweka kiwango cha juu cha wachezaji wanaoweza kufanya mazoezi kwa kila kundi kuwa 14, lakini La Liga iliziambia klabu kuwa zitaruhusiwa kutumia makundi ya wachezaji kumi kila moja.

Advertisement