Julio: Simba, Yanga moto utawaka

KOCHA Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema kwa mwonekano wa vikosi vya Simba na Yanga vinatoa taswira ya namna Ligi Kuu Bara itakakuwa na ushindani msimu huu.

Julio alisema aliona wachezaji wa Simba walivyocheza siku ya tamasha lao la Simba Day dhidi ya Vital’O ya Burundi na kila mmoja alipambana kumshawishi kocha ili kupata namba.

“Unamwona mtu kama Larry Bwalya anavyoonyesha uwezo licha ya ugeni alionao, naamini atasaidia sana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema jambo kubwa wanalopaswa kutambua wachezaji wa timu hiyo ni kutoridhika na mafanikio ya msimu uliopita.

“Yaani mataji ya msimu uliopita, wayasahau waanze kufikiria yaliyopo mbele yao, ili waendelee kufanya vitu vya tofauti katika kizazi chao. Pamoja na Yanga ilikuwa na changamoto ya kukosa kocha mkuu mapema, ilicheza vizuri dhidi ya Aigle Noir, hii inaonyesha msimu huu itakuwa na jipya kwa mashabiki wao, ambao walitamani kuona wachezaji wanaojituma ama wanaoweza kuwapa matokeo,” alisema.

“Klabu hizi zimejiwekea heshima nje ya mipaka yake, lakini haimanishi timu nyingine ni rahisi, bali kongwe zinatakiwa kuwa kioo cha kusajili vizuri na kuonyesha uwezo uwanjani,” alisema Julio akizungumzia msimu mpya unaoanza wikiendi hii.

Yanga itaanzia Dar ikiwakaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa na Simba itakuwa dimba la Sokoine, Mbeya wakikaribishwa na Ihefu