Hamisa awataka wasanii wasameheani

Tuesday April 28 2020

 

By RHOBI CHACHA

MWANAMITINDO nchini,  Hamisa Mobetto amewataka wasanii wenzake kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kuombana msamaha pale walipokoseana na kusameana.
Hamisa ameliambia Mwanaspoti  kuwa amewasamehe watu wote waliomkosea hivyo haoni haja ya wasanii kuendelea kulumbana hasa mwezi huu mtukufu wa toba kwani haileti picha nzuri kwa jamii inayotuzunguka.
“Nawaomba wasanii wenzangu kwa ujumla pamoja na mashabiki zetu tusameheane kwakuwa tunajenga nyumba moja hivyo hatupaswi kugombea fito,” amesema
"Binasfi nimewasamehe wote walionikosea na huwa sipendi kuweka kinyongo moyoni mwangu na ndio maana mtu akinikosea huwa mwepesi kurudisha amani, niko radhi nichekwe lakini amani itawale"amesema Hamisa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni mwezi unaotumiwa na watu wengi katika jamii kuombana msamaha.

Advertisement