Azam chupuchupu kuuvua ubingwa FA

MABINGWA watetezi wa Kombe la FA, Azam FC iliwalazimu kwenda hadi kwenye mikwaju ya penalti  ili kuing'oa African Lyon hatua ya raundi ya tatu ya mashindano hayo.
Azam imesonga mbele  kufuatia kuibuka na ushindi wa penalti  4-1 dhidi ya timu hiyo ya daraja la kwanza baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na Aristica Cioba yaliisaidia Azam  FC  kupata bao la kusawazisha katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe  la FA dhidi ya African Lyon.
Katika kipindi hicho cha pili, Cioba aliamua kumtoa Chirwa nafasi yake aliingia Richard Djodi ambaye alifunga bao hilo la kusawazisha kwa Azam.
African Lyon walionekana kumudu presha ya mashambuzulizi ya Azam  tangu mwanzoni mwa mchezo ambapo walijipatia bao la kuongoza kupitia Mwarami Abdallah.
Mbali na kuingia kwa Djodi ambaye aliisawazishia Azam kwa njia ya faulo, wachezaji wengine ambao waliingia kipindi hicho ni Shaaban Chilunda na  Joseph Mahundi huku wakitolewa Iddy Kipagwile  na Donald Ngoma.
Nidhamu ya ukabaji kwa African Lyon iliwasaidia kuwabana washambuliaji wa Azam kiasi cha kushindwa kuleta madhara kipindi hicho cha pili ambazo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Penalti za Azam katika mchezo huo zilifungwa na Yakubu Mohammed, Djodi, Bruce Kangwa na Shaaban Chilunda, African Lyon walipa moja iliyofungwa na Mwarami huku wakipoteza mbili kupitia Pascal John na Samy Sulutan