Aubemayeng agomea mkataba, Arsenal watafuta njia mbadala

Wednesday March 25 2020

Aubemayeng agomea mkataba, Arsenal watafuta njia mbadala,Klabu ya Arsenal,mshambuliaji  Pierre-Emerick Aubameyang,

 

London, England.Klabu ya Arsenal imeanza mikakati ya kumuuza mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang badaa ya mchezaji huyo kupotezea mazungumzo ya mkataba mpya.

Aubameyang amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, lakini amekatisha mazungumzo ya mkataba wake kabla haya hayajatokea mambo ya ugonjwa wa virusi vya Corona.

Bodi ya Arsenal wanaweka mikakati ya kuhakikisha kwamba mchezaji huyo kama anaondoka basi atoke kabla ya mkataba wake haujamalizika mwakani.

Bodi hiyo wanataka kuhakikisha kwamba Aubameyang atakuwa katika klabu za Ulaya ikiwemo Real Madrid na tayari wameanzisha ajenda hiyo kwa mchezaji Dani Ceballos ambaye yupo kwa mkopo kwenye kikosi chao akitokea Real Madrid ili waweke mazungumzo vizuri katika dili la Aubameyang.

Advertisement