Ambundo ajiweka mkao wa kula

Friday May 15 2020

By THOMAS NG'ITU

MSHAMBULIAJI Dickson Ambundo wa Gor Mahia, amesema katika kipindi hiki ambacho ligi yao imemalizika anaendelea kujiweka fiti kwa kufanya mazoezi ya Gym.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ambundo amesema kwamba imemlazimu kufanya mazoezi hayo kwani hajui ni lini ligi ya Kenya itarejea tena.

"Nataka niwe tayari muda wote na ndio maana naendelea na mazoezi kama kawaida, nafanya Gym ikiwa ni moja ya programu ambazo tulikuwa nayo kabla ya kupewa ubingwa,".

Mshambuliaji huyo aliongeza kwa kusema, licha ya kuwa anafanya mazoezi hayo pia huwa anafanya mazoezi ya kuchezea mpira pamoja na kukimbia.

Ambundo alijiunga na Gor Mahia msimu huu kwa nkopo akitokea katika klabu ya Nyamagana United inayoshiriki Ligi daraja la tatu nchini.

Mkataba wake na Gor unamalizika mwezi wa saba na hivi sasa anasikilizia kuona kama ataendelea kusalia katika kikosi hiko au la.

Advertisement

Katika klabu za nchini aliwahi kuichezea Alliance katika Ligi Kuu msimu wa 2019 kabla ya baadae kuachana na timu hiyo na kurejea katika klabu yake aliyotokea ya Nyamagana United.

Ambundo ajiweka mkao wa kula

SUMMARY:

Dickson Ambundo na David Kissu ni watanzania wanaoichezea klabu ya Gor Mahia.

THOMAS NG'ITU