Nyota Simba, Yanga watawala tuzo mchezaji bora Ligi Kuu

Friday July 31 2020

 

By CLEZENCIA TRYPHONE

WACHEZAJI nane wa Simba na watano wa Yanga ni miongoni mwa wachezaji 30 waliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) wachezaji 30 kutoka timu mbalimbali za ligi iliyofikia tamati wikiendi iliyopita wanawania tuzo hiyo.

Wachezaji wa Simba wanaowania tuzo hiyo ni Shomary Kapombe, John Bocco, Meddie Kagere, Clatous Chama, Francis Kahatta, Jonas Mkude, Luis Miquissone na Aish Manula.

Kwa upande wa Yanga nyota wanaowania tuzo hiyo ni Feisal Salum, Mapinduzi Balama, Deus Kaseke, David Molinga na Juma Abdul.

Wachezaji wa timu nyingine katika Kinyang'anyiro hicho ni Birigimana Blaise, Lucas kikoti na Reliants Lusajo (kutoka Namungo).

Nyota wengine ni David Luhende, Awesu Awesu, Yusuph Mhilu ( Kagera Sugar), Martin Kigi (Alliance), Daluwesh Saliboka (Lipuli) na Marcel Kaheza (Polisi Tanzania).

Advertisement

Pia wapo Nico Wadada, Idd Nado na Obrey Chirwa ( wote kutoka Azam), Abdulmajid Mangalo, Daniel mgore (Biashara United), Ayoub Lyanga na Bakar Mwamnyeto (Coastal Union) na Waziri Junior (Mbao FC).

Wachezaji hao watafanyiwa mchujo baadaye na kubaki 10 kisha watatu ambao wataingia katika kinyang'anyiro kumpata mshindi, tuzo hiyo  itakatolewa Agost 7 mwaka huu katika Ukumbi wa Mliman City, jijini Dar es Salaam.

Advertisement